Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, August 20, 2013

MANCHESTER CITY YAIFUNGA NEWCASTLE 4-0, CITY WAANZA MSIMU MPYA KWA KUGAWA KICHAPO MBELE YA KOCHA WAO MPYA PELEGRINI

Ligi kuu ya nchini Uingereza imeendelea tena leo hii usiku Machester City na Newcastle United, Kocha Manuel Pellegrini wa City akishuhudia timu yake ikitoa kibano cha uhakika na kutimiza yale aliyokuwa akijigamba nayo kuwa anakikosi safi, Yakionekana wazi baada ya wachezaji wake kuifunga bao nne, mbili zikipatikana kipindi cha kwanza na mbili kipindi cha pili kwa timu ya Newcastle inayoongozwa na kocha Alan Pardew usiku huu.

Bao la kwanza likifungwa na Silva dakika ya 6, huku mchezaji matata  Aguero akimalizia bao la pili dakika ya 22 dhidi ya Newcastle, huku Newcastle wakiambulia mwenzao Taylor akipewa kadi nyekundu baada ya kumfanyia ndivyo sivyo Sergio Aguero huku akiwa na  kadi ya njano aliyopewa mapema katika kipindi hiki cha kwanza. Kipindi cha pili pia hakikupishana sana na kipindi cha kwanza City wameanza na machachali sana na kufanikiwa kupata bao la tatu kupitia mchezaji Toure kwa kupiga frii kiki kuelekea golini dakika ya 50. Dakika ya 75 mchezaji Nasri akipewa pasi safi akawachomoka mabeki wa Newcastle na kuipachikia bao la nne City na kufanya 4-0 dhidi ya timu ya Newcastle.Manchester City kipindi hiki cha pili pia wametumia mwanya wa wachezaji pungufu wa Newcastle na kuutumia vizuri huku wakiwashambulia na kufika mara nyingi kwenye lango la Newcastle.
Sergio Aguero akichonga ...hapa na kutupia!!  David Silva ndiye aliyeanza kufunga bao
Silva akishangilia baada ya kufunga!!
Aguero cakishangilia baada ya kufunga bao..  Mchezaji Steven Taylor akifanyia majanga mchezaji wa City Sergio Aguero hapa na kupewa kadi nyekundu.
Refa Andre Marriner Steven Taylor akimwonesha kadi nyekundu Toure akishangilia kimya kimya baada ya kuifunga timu ya Newcastle bao la tatu. Kocha Manuel Pellegrini akiongea na Samir Nasri kabla ya kuingia uwanjani kuchukua nafasi ya Sergio Aguero.
Samir Nasri akifunga bao la mwisho na kufanya 4-0 dhidi ya NewcasleNasri akishangilia baada ya kufunga bao la 4
VIKOSI:
Manchester City: Hart, Zabaleta, Kompany, Lescott, Clichy, Fernandinho, Toure, Jesus Navas, Aguero (Nasri 61), Silva, Dzeko.
Subs: Milner, Negredo, Kolarov, Javi Garcia, Rodwell, Pantilimon.
Booked: Dzeko, Fernandinho.
Goals: Silva 6, Aguero 22, Toure 50, Nasri 75.

Newcastle United: Krul, Debuchy, Coloccini, Steven Taylor, Yanga-Mbiwa, Sissoko, Tiote, Gouffran (Dummett 45+4), Ben Arfa, Gutierrez (Anita 44), Cisse.
Subs: Elliot, Marveaux, Shola Ameobi, Obertan, Sammy Ameobi.
Booked: Yanga-Mbiwa, Sissoko, Debuchy.
Sent off: Taylor.

Referee: Andre Marriner (W Midlands)

No comments:

Post a Comment