Mkufunzi wa kozi hiyo ni Govinder Thondoo kutoka Mauritius. |
Makocha 32 kutoka mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani wanashiriki kozi ya Copa Coca-Cola inayoanza kesho (Agosti 12 mwaka huu) jijini Dar es Salaam chini ya Mkufunzi kutoka Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Mpira wa Miguu (FIFA).
Kozi hiyo itakayomalizika Agosti 17 mwaka huu itafunguliwa saa 3 kamili asubuhi kwenye ukumbi wa Msimbazi Centre na washiriki wote tayari wameshawasili Dar es Salaam. Mkufunzi wa kozi hiyo ni Govinder Thondoo kutoka Mauritius.
Washiriki wa kozi hiyo ni Ahazi Ibrahim Kasegese (Mbeya), Aloyce Mayombo (Pwani), Andrew Zoma (Tabora), Asuri Msakamali (Simiyu), Bakari Khamis Kilambo (Kaskazini Pemba), Chacha Sambulo (Mara), Charles Rwezaura (Kagera), Daniel Sambala (Njombe), Dudu Haruni (Iringa) na Emmanuel Kapurata (Rukwa).
Faki Makame Haji (Kaskazini Unguja), Fatawi Khamis Sheha (Kusini Pemba), Hamisi Omary Mabo (Kigoma), Hussein Maulid (Morogoro), Issa Lugaza (Kilimanjaro), James Gaspar (Shinyanga), James Wambura (Arusha), Jomo Jackson Puccey (Lindi), Joseph Sihaba (Dodoma), Kelvin Haule (Ruvuma) na Kessy Juma Abdallah (Tanga).
Kessy Mziray (Mwanza), Menswi Mchwampaka (Kinondoni), Mohamed Abdallah Kweka (Singida), Nurdin Gogola (Temeke), Pius Kamande (Rukwa), Ramadhan Abrahman Ramadhan (Mjini Magharibi), Ramadhan Salum Mnyoti (Manyara), Raphael Ngeleja (Geita), Samuel Edgar Maokola (Ilala), Shaweji Nawanda (Mtwara) na Vuai Abdul Haji (Kusini Unguja).
Fainali za U15 Copa Coca-Cola ngazi ya Taifa zitafanyika Septemba mwaka huu jijini Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment