Rais wa TPBO LIMITED Yassini Abdallah 'Ostadhi' akimkabizi mkataba wa makubaliano bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' baada ya kutia saini jana katika ofisi za TPBO LTD Dar es salaam |
Rais wa TPBO LIMITED Yassini Abdallah 'Ostadhi' akimkabizi mkataba wa makubaliano bondia Simba Watunduru baada ya kutia saini jana katika ofisi za TPBO LTD Dar es salaam |
Rais wa TPBO LIMITED Yassini Abdallah 'Ostadhi' kushoto akimwangalia bondia Simba Watunduru anavyo usoma mkataba wake kabla ya kutia saini Dar es salaam jana |
Rais wa TPBO LIMITED Yassini Abdallah 'Ostadhi' kushoto akimwangalia bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akitia saini mkataba wake Dar es salaam jana |
Mabondia Simba Watunduru kushoto na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakitunisha misuli wakati wa kupiga picha kwa ajili ya kutangaza mpambano wao |
Mabondia Simba Watunduru kushoto na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakitunishiana misuli wakati wa kutangaza mpambano wao |
KING CLASS MAWE |
Akizungumzia tukio hilo rais huyo alisema sijawahi kuona vitu kama hivi vya ajabu mana vijana wamekamiana mpaka kufikia hatua ya kuchapana kavu kavu mbele yangu hata hivyo mzozo huo umekubaliana kumalizika siku ya mpambano wao ambapo atajulikana nani mbabe zaidi ya mwenzake
Nae bondia Ibrahimu Class aliyeanzisha mzozo huo ameaidi kumaliza mapema mpinzani wake ambapo anatarajia kumchakaza raundi za awali na bondia Simba amejigamba kumchapa Class kwa KO
Wakati wowote ule unajua huyo ni kijana mdogo sana mmeuwaisha kwangu sasa siku hiyo mimi nitampiga KO mbaya sana najua kuwa kwa Tanzania hii mimi ndie naongoza kuwapiga wapinzani wangu kwa KO pindi nikutanapo ulingoni
No comments:
Post a Comment