Mechi hii ya Kirafiki
ikichezwa bila Kiungo Michael Carrick ambae ni Kiungo wa Manchester United mwenye Miaka 32,
amelazimika kujiondoa baada ya Jicho lake moja kupata ugonjwa. England usiku huu wakicheza na Mahasimu wao wakubwa
Scotland ambao hawajakutana nao tangu Novemba 1999.
Scotland ndio walianza
kuziona nyavu za England kupitia mchezaji wao James Morrison dakika ya 11.
Baadae dakika ya 29 Walcott akapenyeza kwenye ngome ya Scotland na kuwapita
mabeki na kufunga bao safi. Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinaisha timu
zote zilikuwa zinalingana zikiwa na bao 1-1.


Kipindi cha pili
dakika ya 50 mchezaji wa Scotland Miller
akawapatia bao na kufanya 2-1. England wakaongeza mashambulizi na kuweza
kusawazisha bao hilo dakika tatu mbele mchezaji anayeichezea Manchester United
Welbeck dakika ya 53
akasawazisha na kufanya 2-2. Dakika ya 70 mchezaji Lambert aliyeingia kipindi cha pili anaunganisha pasi safi kwa kichwa na kuipatia bao la 3
na la ushindi England dhidi ya Mahasimu
wao wakubwa Scotland.
Mechi hii ya England v Scotland ni sehemu ya Sherehe za FA, Chama cha Soka England kusheherekea Miaka 150 ya uhai wake na Mechi hii itakuwa ya 111 kati ya Mataifa hayo, ya kwanza ilikuwa Mwaka 1872 na baada ya hapo walikutana kila Mwaka hadi 1989.

Mechi hii ya England v Scotland ni sehemu ya Sherehe za FA, Chama cha Soka England kusheherekea Miaka 150 ya uhai wake na Mechi hii itakuwa ya 111 kati ya Mataifa hayo, ya kwanza ilikuwa Mwaka 1872 na baada ya hapo walikutana kila Mwaka hadi 1989.














VIKOSI:
England: Hart, Walker, Cahill, Jagielka, Baines, Cleverley (Milner 67), Gerrard (Oxlade-Chamberlain 62), Wilshere (Lampard 46), Walcott, Rooney (Lambert 67), Welbeck.
Subs: Foster, Johnson, Cole, Jones, Smalling, Defoe, Zaha, Ruddy.
Goal: Walcott 29, Welbeck 53, Lambert 70.
Booked: Walker, Walcott.
Scotland: McGregor, Hutton, Martin, Hanley, Whittaker, Snodgrass (Conway 67), Morrison, Brown, Forrest (Mulgrew 67), Maloney, Miller.
Subs: Gilks, McArthur, Naismith, Burke, Adam, Webster, Rhodes, Bannan, Griffiths, Mackay-Steven, Dorrans, Boyd, Greer, Hammell, Marshall.
Goal: Morrison 11, Miller 50.
Booked: Snodgrass.
Referee: Felix Brych (Germany)
No comments:
Post a Comment