Didier Drogba ameitwa tena katika kikosi cha timu ya taifa ya Ivory Coast ikiwa ni kwa mara ya kwanza tangu alipoachwa mapema mwaka huu.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 35 ameorodheshwa katika kikosi cha wachezaji 23 kuelekea katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Mexico mjini New York Agosti 14.
Drogba aliachwa kwa mara ya kwanza na kocha Sabri Lamouchi mara baada ya michuano ya mataifa ya Afrika kuelekea katika michezo ya kuwania kufuzu kombe la dunia katika miezi ya Machi na Juni.
Wakati huo Lamouchi alisisitiza kuwa Drogba alipaswa kuongeza uimara wake
Drogba alihangaika wakati wakati wa michuano ya mataifa ya Afrika ambayo Ivory Coast iliyokuwa ikipewa nafasi kubwa kutwaa michuano hiyo ilichapwa katika mchezo wa hatua ya robo fainali na walionyakuwa ubingwa huo Nigeria.
Drogba, ambaye ana matumaini ya kutokeza tena kwa mara ya tatu katika fainali za kombe la dunia nchini Brazil mwakani alionyesha makali yake mwishini mwa juma wakati wa mchezo wa maandalizi ya kuanza msimu kwa kuisaidia timu yake ya Galatasaray kushinda mchezo dhidi ya Arsenal.
Lamouchi pia aamewaita kwa mara ya kwanza mshambuliaji wa Anderlecht Zoro Cyriac Gohi Bi na kiungo mpya wa Malaga Bobley Anderson hii ikiwa imethibtishwa ndani ya taarifa iliyotolewa na shirikisho la soka la nchi hiyo IFF. Ivory Coast squad to face Mexico:Goalkeepers: 1 Boubacar Barry (Lokeren, Belgium), Badra Ali Sangare (Ivoire Academie, Ivory Coast)Defenders: Jean-Daniel Akpa-Akpro(Toulouse, France), Benjamin Angoua (Valenciennes, France),Serge Aurier (Toulouse, France), Souleman Bamba (Trazbonspor, Turkey), Arthur Boka (Stuttgart, Germany), Viera Darrassouba (Caykur Rizespor, Turkey), Brice Dja Djedje (Evian, France), 10 ZOKORA Didier (Trazbonspor, Turkey),Midfielders: Bobley Anderson (Malaga, Spain), Jean-jacques Gosso-Gosso (Glençlerbirligi SK, Turkey), Abdul Razak (Manchester City, England), Geoffrey Serey Die (Bale, Switzerland), Giovanni Sio (Wolsburg, Germany), Cheikh Tiote (Newcastle, England), 17 Yaya Toure (Manchester City, England),Forwards: Mathis Bolly (Dusseldorf, Germany), Wilfried Bony (Swansea, England), Gervinho (Arsenal, England), Didier Drogba (Galatasaray, Turkey), Salomon Kalou (Lille, France), Cyriac Gohi bi Zoro (Anderlecht, Belgium)
No comments:
Post a Comment