MANCHESTER CITY KUMSAJILI ALVARO NEGREDO WA SEVILLA KUZIBA PENGO LA CARLOS TEVES
Manchester City imeonyesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa Sevilla ya Hispania Alvaro Negredo kuziba nafasi ya Carlos Tevez baada ya kutimkia Juventus.Negredo mwenye umri wa miaka 27, amekadiriwa kwa thamani ya pauni milioni 24 huku City wakiwa na matumaini ya kumnasa kwa thamani pungufu ya hiyo.Atletico Madrid walikuwa na mpanago wa kumchukua Negredo, lakini meneja mpya wa City Manuel Pellegrini ameweka wazi kuwa huyo ndiye mchezaji satahili kuziba pengo la Tevez.Everton na West Ham hivi karibuni nao walikuwa wameonyesha nia lakini mshambuliaji huyo alidhihirisha kuwa ni wa thamni kubwa kwa vilabu vyote viwili.Fernandinho na Jesus Navas tayari wameshawasili wakitoka katika vilabu vya Shakhtar Donetsk na Sevilla majira haya ya kingazi wakati City wakiimarisha kikosi chao kwa ajili ya kuchukua taji la ligi kuu ya England waliloliacha kwa Manchester United msimu uliopita.Manchester City pia imekuwa ikihusihswa na mshambuliaji wa Benfica Oscar Cardozo katika harakati zao za kuimarisha kikosi chao katika sehemu ya ushambuliaji baada ya kumuuza Mario Balotelli alielekea AC Milan ya Italia mwezi Januari.Sergio Aguero amekubali mpango wa muda mrefu na Etihad, wakati ambapo inaaminika kuwa Pellegrini anataka kufanya kazi na Edin Dzeko ambaye hakuwa na wakati mzuri chini ya meneja aliyetangulia Roberto Mancini msimu uliopita.
No comments:
Post a Comment