Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, July 22, 2013

JOHN TERRY HAYUPO SALAMA CHELSEA, REINA WA LIVERPOOL AJIUNGA NA NAPOLI KWA MKOPO NA MLINZI WA ARSENAL ANDRE SANTOS ASAJILIWA NA FLAMENGO YA BRAZIL


John Terry hayuko salama Chelsea, anasema  Jose Mourinho
Meneja wa Chelsea Jose Mourinho amesisitiza kuwa nahodha wkae John Terry hayuko sawa na kwamba atatakiwa kudhihirisha ubora wake katika kikosi cha kwanza ndani ya mkataba wake.
Terry mwenye umri wa miaka 32 alikuwa ni skipper muhimu katika kikosi cha Mourinho kuanzia mwaka 2004 mpaka 2007 na kwasasa amesaliwa na mwaka mmoja ndani ya mkataba wake.
Mourinho amesema
 "Hayuko sawa na mwenyewe anajua kuwa hayukoa sawa. Kitu pekee anachojua ni juu ya urafiki wake lakini kiutaalamu hakuna aliye sawa.
Terry akitwaa mataji chini ya Mourinho
    Premier League (2): 2004-05, 2005-06
    FA Cup (1): 2006-07
    Football League Cup (2): 2004-05, 2006-07
    FA Community Shield (1): 2005

Pepe Reina wa Liverpool kujiunga na Napoli kwa mkopo
 Mlinda mlango wa Liverpool Pepe Reina anajipanga kujiunga na Napoli kwa mkopo wa muda mrefu.
Kocha wa Napoli Rafael Benitez amekuwa akimkufukuzia Mhispania mwenzake huyo ambaye alikuwa nambari moja kipindi chake Anfield, baada ya kushindwa kumnasa mlinda mlango wa QPR Julio Cesar.
Reina mwenye umri wa miaka 30, alitarajiwa kurejea mazoezini katika klabu yake Jumapili kwa kujiunga na wachezaji wenzake huko katika ziara ya maandalizi ya msimu.
Liverpool ilimsainisha mlinda mlango raia wa Belgium Simon Mignolet kutoka katika klabu ya Sunderland kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni £9 mwezi uliopita.
Reina alijunga na Liverpool akitokea Villarreal mwaka 2005.

Flamengo ya Brazil yamsajili kwa mkataba wa kudumu mlinzi wa Arsenal Andre Santos.
 Arsenal imemuuza mlinzi wake wa kushoto Andre Santos katika klabu ya Flamengo ya nchini Brazil.

Mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 30 alijung a Gunners akitokea Fenerbahce  ya Uturuki kwa ada ya wakati huo ya pauni milioni £6.2 mwezi August 2011 lakini alishindwa kuonyesha ubora wa soka yake ndani ya klabu hiyo

Andre Santos at Arsenal
Appearances: 33
Goals (all competitions): 3

Alirejea katika taifa lake la Brazil na kujiunga na Gremio kwa mkopo mwezi January 2013 kufuatia Arsenal kumsajili mlinzi mwingine wa kushoto Nacho Monreal kutoka katika klabu ya Malaga.
Santos ambaye alikuwa kwa mkopo katika klabu ya Flamengo katika msimu wa 2005-06 sasa anajiunga nao tena kwa mkataba wa kudumu.
Taarifa ya klabu ya Arsenal kwa njia ya mtandao imearifu kuwa "Kila mtu ndani ya Arsenal angependa kumshukuru Andre kwa mchango wake ndani ya klabu na anamtakia kila la kheri huko baadaye"
Ameichezea Arsenal michezo 33 na kuifungia mabao matatu .

No comments:

Post a Comment