Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, July 5, 2013

ILALA NA KINONDONI KUCHEZA FAINALI YA AIRTEL RISING STARS KWA UPAND WA WASICHANA

TIMU za wanawake za Ilala na Kinondoni zimefuzu fainali ya mashindano ya Airtel Rising Stars zinazochezwa Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.

Ikicheza kwa ustadi mkubwa timu ya Kinondoni iliweza kuibugiza bila huruma timu ya mkoa wa Kigoma kwa mabao 7-0 katika mechi ya asubuhi.

Mabao ya ushindi yaliwekwa kimiani na wachezaji Sherida Boniface aliyefunga mabao manne katika dakika za 10, 14, 6, 38 na mabao mengine yalifungwa na Tatu Iddi dakika ya 7, Shamimu Khamisi dakika 23 na Christina Daudi dakika ya 40.

Katika mechi ya pili iliyo wakutanisha timu za Ilala na Temeke, Ilala ilifanikiwa kutinga fainali baada ya kuichapa Temeke kwa mikwaju ya penati 2-0 baada ya kutoshana nguvu ya bao 1-1 katika muda wa kawaida.

Mabao katika muda wa kawaida kwa timu ya Temeke lilifungwa na Donisia Daniel dakika 32 na Neema Paul wa Ilala alisawazisha bao hilo dakika 50 na kufanya matokeo kuwa 1-1 hadi dakika 90


Kwa upande wa penati waliopata kwaupande wa Ilala ni Maimuna Khamis, Donisia Daniel na Modisine Sylvester alipoteza huku Temeke  wapigaji wake wote walikosa ambao ni Mwantumu Ramadhani, Amina Ramadhani, Neema Paul na Arafa Abdul.




No comments:

Post a Comment