Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, July 8, 2013

GHANA WAIBANA CHILE KWA DAKIKA 120, WAIFUNGA 4-3 NA KUTINGA NUSU

GHANA, Nchi pekee ya Afrika kutwaa Kombe la Dunia U-20 Mwaka 2009, Jana Usiku huko Turkey, iliwabwaga Chile Bao 4-3 baada Dakika 120 za Robo Fainali ya ya Mashindano ya FIFA ya Kombe la Dunia kwa Vijana chini ya Miaka 20, U-20.

Hadi Dakika 90 kumalizika matokeo yalikuwa Ghana 2 Chile 2.

Ghana walipata Bao la kwanza katika Dakika ya 11 baada ya Frank Acheampong kumtengenezea Moses Odjer alieweka kifuani na kuachia shuti kali lakini Chile walijibu kwa Bao 2 za haraka za Nicolas Castillo na Mchezaji wa Manchester United Angelo Henriquez kwenye Dakika za 23 na 27. 

Ghana walifanya Gemu kuwa 2-2 katika Dakika ya 72 kwa Bao la Ebenezer Assifuah na Mechi kuingia Dakika za Nyongeza 30.

Katika Dakika ya 98, Angelo Henriquez aliipeleka Chile kuwa 3-2 lakini Seidu Salifu akaisawazishia Ghana katika Dakika ya 113 na Assifuah kuipa ushindi kwa Bao la 4 katika Dakika ya 120.


MAGOLI:
Ghana 4
-Dakika ya 21 Odjer
-72 & 120 Assifuah
-113 Salifu
Chile 3
- Dakika ya 23 Nicolas Castillo
-27 & 98 Angelo Henriquez

Katika Robo Fainali iliyotangulia Jana Usiku, Iraq mara 3 waliongoza lakini mara zote South Korea walisawazisha kwenye Mechi ambayo ilimalizika Bao 2-2 katika Dakika 90 na kuongezwa Dakika za Nyongeza 30.
Katika Dakika hizo za Nyongeza, Iraq walifunga Bao lao la 3 katika Dakika ya 118 lakini katika Dakika ya mwisho ya muda wa majeruhi, South Korea walisawazisha katika Dakika ya 122 na ndipo ikaja Tombola ya Mikwaju ya Penati ambazo Iraq walishinda kwa Penati 5-4 wakati South Korea walipokosa Penati 2 na Iraq 1.

MAGOLI:
Iraq 3
-Dakika ya 21 Atiyah Ali Faez
-42 & 118 Farhan
South Korea 3
- Dakika ya 25 Kwon Chang Hoon
-50 Lee Joo-Young
-122 Jung

Nusu Fainali zitachezwa hapo Jumatano Julai 10 kwa France kucheza na Ghana kisha kufuatia Iraq v Uruguay.
Fainali ni Jumamosi Julai 13.


RATIBA/MATOKEO:
ROBO FAINALI
45      06/07 France 4 Uzbekistan 0
46      06/07 Uruguay 1 Spain 0
47      07/07 Iraq 3 South Korea 3 [Dak 120 3-3, Iraq Washindi Penati 5-4]
48      07/07 Ghana 2 Chile 2 [Dakika 120, Ghana 4 Chile 3]
NUSU FAINALI
49      10/07 18:00 Bursa France v Ghana
50      10/07 21:00 Trabzon Iraq v Uruguay
MSHINDI WA TATU
51      13/07 18:00 Istanbul L49 v L50

No comments:

Post a Comment