Uganda Cranes imejiweka katika nafasi nzuri leo katika kufuzu kombe la dunia 2014 baada ya kuifunga Liberia bao 1-0 katika Uwanja wa Mandela jijini kampala.
Mechi hiyo iliiisha vibaya baada ya wachezaji wa Liberia wakiongozwa na nyota wao Roberts Omega kumzonga mwamuzi wa mchezo Adam Cordier kutoka Chad kwa kile walichodai kuchezesha vibaya kiasi cha kuwafanya wa kushindwa kuvumulia benchi la ufundi ilibidi wapunguze hasira ili kutuliza vurugu hizo.
Goli la ushindi liliwapa mashabiki wa Uganda hari ya juu mara baada ya Tonny Mawejje kufunga goli katika dakika ya sita ya mchezo, goli lililopatikana baada ya kuidanganya safu ya ulinzi ya Liberia na kuachia shuti kali huku safu ya ulinzi isijue cha kufanya.
Uganda kwa sasa ina pointi 5 sawa na Senegal ambao nao wanacheza na Angola huko Luanda katika kundi J. Timu zote zina alama 5 huku Liberia ikiwa na alama 4 wakati Angola wao wana alama 3.Timu inayoongoza kwa kila kundi itafuzu kwa hatua ya pili ya mtoano.
No comments:
Post a Comment