Ni vita baina ya Tottenham na Liverpool wakimtaka Henrikh Mkhitaryan (kushoto pichani) akitokea Shakhtar Donetsk. |
Bosi wa Anfield Brendan Rodgers ameonekana kuwa kinara wa kukamilisha usajili wa mchezji huyo ambaye anaonekana kuwa ni mwenye kipaji ilhali Spurs kwasasa nao wanaonekana kuwa mbionioni kumnasa nyota huyo wa kimataifa wa Armenia.
Imefahamika kuwa mshauri wa Mkhitaryan amekuwa katika mazungumzo na wakuu wa Tottenham juu ya kusaka uwezekano wa kumpeleka White Hart Lane msimu ujao.
Spurs kwasasa pia wako katika mpango wa kumkamata Puulinho wa Corinthians kwa ada ya uhamisho wa pauni milioni £17 ambaye anatazamiwa kukamilisha mipango ya kuanguka saini baada ya fainali ya michuano ya kombe la mabara hapo kesho Jumapili.
Taarifa nyingine zinasema washindi wa pili wa ligi ya mabingwa Ulaya Borussia Dortmund nao wameweka mezani pauni milioni £19.5 kwa ajili ya kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24.
Lakini Shakthar wamesisitiza kuwa wanahitajia angalau pauni milioni £25 kwa ajili ya mchezaji huyo ambaye anatakiwa na vilabu vya England kama vile Chelsea na Manchester City.
Spurs wanasalia na matumaini mengine ya kumchukua David Villa pamoja na mshambuliaji mwingine wa Galatasaray Burak Yilmaz mwenye umri wa miaka 27.
No comments:
Post a Comment