Mabingwa soka katika bara la Afrika, Nigeria wameiondoa Malawi katika uongozi wa kundi lao kwenye michuano ya kufuzu kombe la dunia baada ya kuifunga Kenya bao 1-0 katika jiji la Nairobi.
Ahmed Musa ndiye aliyepeleka kilio kwa mashabiki wa Kenya zikiwa zimesalia dakika tisa mchezo kumalizika na kuwapa tai hao wa kijani alama mbili zaidi za uongozi dhidi Malawi na kuongoza kundi F baada ya mechi Nne.
Malawi imetoka suluhu ya kutofungana na Namibia, mchezo uliopigwa mjini Blantyre ambapo Malawi ndio walikuwa wenyeji. Malawi ambao walikuwa wakilingana alama na Nigeria kabla ya mechi ya leo.
Mpaka sasa Kenya haijashinda mechiyeyote ila imetoka suluhu mbili, wakati Namibia, wana alama nne, ambao wanasalia katika nafasi ya tatu.
Mechi hii ya leo imewahi kuchezwa kutokana na Nigeria kukabiliwa na mashindano ya mabara yanayotaraji kuanza Brazil Juni 15 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment