Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, June 5, 2013

NGWEA AAGWA LEADERS CLUB LEO, VITUKO VATAWALANA KUSAFIRISHWA KWENDA MOROGORO

Wakazi wa jijini Dar es Salaam, leo wamejitokeza kwa wingi kwenye Viwanja vya Leaders Club Kinondoni, kwa ajili ya kuaga mwili wa marehemu Albert Mangwea, aliyefariki Mei 28, nchini Afrika ya Kusini.

Mwili wa Mangwea  uliwasili nchini jana machana ambapo leo shughuli ya kuagwa mwili huo imekamilika majira ya saa saba mchana na kuanza safari ya kuelekea mjini Morogoro kwa maziko.
Shughuli hiyo imehudhuriwa na wananchi mbalimbali, Wasanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Wasanii wa filamu na baadhi ya Viongozi wa Serikali na wa Vyama vya Siasa.

Baada ya kukamilika kwa shughuli hiyo, wananchi ambao asilimia kubwa waliokuwapo viwanjani hapo walikuwa ni vijana, walitoa kali ya mwaka pale walipomzonga msanii wa muziki wa kizazi kipya Diamond, kama nyuki wakati akiondoka viwanjani hapo na kuzua hofu kwa baadhi ya watu waliokuwapo eneo hilo wakizani lilikuwa ni tukio la hatari kutokana na jinsi kundi hilo la vijana lilivyokuwa likitawanyika kwa staili ya kutimka viwanjani hapo.

Msanii mwingine, aliyezongwa na vijana hao ni Mr. Blue, pamoja na Kitale, ambaye alizongwa hadi kuibiwa simu yake ya mkononi na kama ilivyo kawaida yake awapo katika Sini za Filamu, alimkamata mwizi wake na kumpakia katika gari lake na kuondoka naye kusikojulikana na kuwaacha watu hoi huku wakiangua vicheko na kuona kama alikuwa akiigiza.
Jeneza la mwili wa Mangwea, likiondolewa viwanjani hapo baada ya kuagwa.
 Sehemu ya wananchi waliojitokeza kuaga mwili wa marehemu Mangwea........
 P. Funky akipita kuaga na kutoa heshima za mwisho mbele ya jeneza la Mangwea
 Wanafamilia wakipita kuaga mwili wa ndugu yao....
 Sehemu ya wanafamilia.....
 Huyu naye ambaye haikuweza kufahamika jina lake kwa haraka, akipiga picha huku akiangua kilio wakati wa kuaga mwili wa marehemu.....

 Jeneza likiondolewa kupelekwa kupakiwa kwenye  gari tayari kuanza safari ya kuelekea Morogoro.
 Sehemu ya wanafamilia wakiaga.....
 Wengine walikuwa vituko viwanjani hapo kama jamaa huyu anavyoonekana akinywa Bia, huku akiwa na sigara mkononi na pia akipiga picha kwa kutumia simu yake, huku akiwa amebeba Gitaa lake.

Ndiyo huyu huyu tena hapa akinasa kumbukumbu ya jeneza huku akilia.....sasa sijui ilikuwa ni ile Biere aliyokuwa akinywa ama ni machungu ya kweli......
 Mboto naye akiwasili viwanjani hapo....
 Lady Jay Dee pia alikuwa ni mmoja kati ya wasanii waliokuwapo viwanjani hapo.....
 Hii ndiyo Kamati ya maandalizi ya kufanikisha shughuli hiyo.....
 Wengine pia walikuwa ni vituko kwa aina ya mavazi, kama mwandishi huyu alionekana akiwa ametinga nguo inayomuonyesha mwili wake.....
 Heshima za mwisho....
 TID akihojiwa kuhusiana na msiba huo.....
 Jay Moe, akizungumza Live na kituo cha Redio kutoka viwanjani hapo.....
 Wasanii wakipita kutoa heshima za mwisho.....
 Baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya na wasanii wa Filamu, waliojitokeza kwenye shughuli hiyo..
 Baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya na wasanii wa Filamu, waliojitokeza kwenye shughuli hiyo..
 Baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya na wasanii wa Filamu, waliojitokeza kwenye shughuli hiyo..
 Baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya na wasanii wa Filamu, waliojitokeza kwenye shughuli hiyo..
 Dj Choka, akimshikilia msanii wa muziki wa kizazi kipya, Q-Chillah, aliyekuwa akiangua kilio baada ya kupita na kutoa heshima zake za mwisho mbele ya Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Mangwea....
 Baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya na wasanii wa Filamu, waliojitokeza kwenye shughuli hiyo..
 Baadhi ya wanafamilia wakisubiri kutoa heshima za mwisho.....
 Baadhi ya wanafamilia wakisubiri kutoa heshima za mwisho.....
 Sehemu ya wananchi wakiwa kwenye foleni ya kuaga......
 Askari Polisi wakituliza ghaasia zilizokuwa zikitokana na wananchi waliokuwa wakijaribu kuwahi foleni...
 Mbunge wa Konondoni, Idd Azan, akiongoza kuaga......na kutoa heshima za mwisho.....
 Wasanii wakiwa kwenye foleni ya kwenda kuaga......
 Msanii Keisher, akipita kutoa heshima za mwisho.....
 Gadna G Habash, akiongoza shughuli hiyo....
 Mzee Magari na wasanii wa Filamu wakipita kutoa heshima za mwisho......
 Mheshimiwa Temba akipita kuaga....
 Polisi Jamii wakiranda na mbwa kudhibiti vurugu.....
 G Habash akizungumza .....
 Wasanii wakipita kuaga.....
 Msanii Dogo Hamidu, akipiga saluti ........
 Msanii wa kundi la The Comedy, Joti, akipita kutoa heshima zake za mwisho...
 Vijana wakifukuza gari la Msanii Mr. Blue wakitaka asimame ili wamzonge kama walivyofanya kwa Diamond.....

No comments:

Post a Comment