Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, June 10, 2013

KOCHA WA TIMU YA TAIFA YA NAMIBIA AJIUZULU KWA SABABU YA VITISHO VYA KUUWAWA


Roger Palmgren ameamua kuachana na kazi ya kuifundisha timu ya taifa ya Namibia kufuatia yeye na familia yake kupokea vitisho vya kuuwawa.
Rais wa shirikisho la soka la Namibia John Muinjo amesema "Roger ametutumia ujumbe wa barua pepe akisema maisha yake yapo hatarini kwani amepokea vitisho na kwa msingi huo ameamua kujiuzulu"“Nimekuwa katika soka kwa muda mrefu nimeshudia makocha wakiajiriwa na kufukuzwa lakini sikuwahi kushuhudia hili likitokea”

Roger hakushirikiana na sisi kuhusi jambo hili hivyo hatukuweza kulishughulikia kujua ni nani anahusika, hatukuwa na mazungumzo naye".
"Hatukuwahi kuwa na tatizo hilo huko nyuma ninaogopa endapo itakuwa kweli. Sina hakika kwa asilimia 100% kama ni kweli, Itakuwa vizuri kama tungelifanyia uchunguzi"

Kujiuzulu kwa kocha huyo raia wa Sweden kunafuatia masaa 48 kabla ya timu ya taifa ya Namibia maarufu kama 'Brave Warriors' haijawakaribisha vinara wa kundi F Nigeria katika mchezo ambao kwao ni lazima kushinda ili kuwepa veam kampeni ya kufuzu kucheza kombe  la dunia 2014.

Namibia inahitaji kujikusanyia zaidi alama ili kuweka hai matumaini yao ya kufuzu wakiwa na nafasi finyu ya kuingia katika timu za mwisho zitakazo cheza michezo ya mtoano yaani play-off round kuamua watakao fuzu fainali za nchini Brazil mwakani.

Kocha huyo wa zamani wa Sierra Leone na Rwanda Palmgren, mwenye umri wa miaka 50, alichukua nafasi hiyo mwezi uliopita na mchezo wake wa kwanza wa kimashindano ulikuwa nchini Malawi ambapo walikwenda sare 0-0 na wenyeji wao katika kampeni ya kufuzu kombe la dunia.

Kocha msaidizi Ricardo Mannetti na Ronnie Kanalelo wanachukua nafasi ya kukinoa kikosi cha Namibia kuelekea katika mchezo dhidi ya Nigeria.

No comments:

Post a Comment