Kala Jeremiah akielekea kuchukua tuzo yake huku akisindikizwa na mtayarishaji wa nyimbo yake ya Wimbo Bora wa Mwaka (Dear God)
Kala Jeremiah akiwasahukuru mashabiki wake baada ya kupokea tuzo yake.
Kala Jeremiah akiwasahukuru mashabiki wake baada ya kupokea tuzo yake.
Meneja Masoko wa TBL, Kushila Thomas akimkabidhi tuzo
Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), David Mgwassa akimkabidhi tuzo mtoto wa marehemu Salum Abdallah.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe akikabidhi tuzo ya msanii Bora wa kiume wa mwaka kwa mwakilishi wa msanii Diamond Platnumz.
Ommy Dimpoz akipokea tuzo yake ya wimbo bora wa mwaka
kutoka kwa Wema Wepetu. Wimbo wa Me n U - Ommy Dimpoz Feat Vanessa Mdee ndio ulioshindaniwa na kuibuka kidedea.
Ommy Dimpoz akiwashukuru mashabiki wake. Wa pili kushoto ni Vanessa Mdee.
Ommy Dimpoz akiwashukuru mashabiki wake. Wa pili kushoto ni Vanessa Mdee.
DAR ES SALAAM, Tanzania
HATIMAYE kitendawili cha nani kavuna nini katika kinyang’anyiro Kilimanjaro Tanzania Music Awards KTMA 2013, kilipata jibu usiku wa jana, ambapo kategori 37 za mchakato huo zilipata washindi, huku wasanii Kala Jeremiah na Ommy Dimpoz wakifunika kwa upande wa muziki wa kizazi kipya.
Kala Jeremiah aliyekuwa karibu atwae tuzo, alijikuta akimaliza kwa kutwaa tuzo tatu za Wimbo Bora wa Mwaka (Dear God), Msanii Bora wa Hip Hop na ile ya Mtunzi Bora Bora wa Hip Hop, huku akiipoteza ya Wimbo Bora wa Mwaka wa Hip Hop(Dear God) iliyochukuliwa na Nay wa Mitego kuptia wimbo Nasema Nao.
Kwa upande wa Dimpoz, nyota pekee aliyekuwa akiwania tuzo saba katika kinyang’anyiro hicho, alipata tuzo tatu za Wimbo Bora wa Bongo Pop (Me and You feat Vanessa Mdee), kibao kilichompa pia tuzo ya Wimbo Bora wa Ushirikiano.
Dimpoz akapokea tuzo ya tatu ya Video Bora ya Mwaka kupitia kibao cha Baadae,huku akiangukia pua katika kategori nne za Wimbo Bora wa Mwaka, Msanii Bora wa Mwaka wa Kiume, Msanii Bora wa Mwaka wa Kiume – Bongo Flava na Mtunzi Bora wa Mashairi – Bongo Flava.
Katika namna iliyowavutia wengi, Dimpoz aliitoa kwa Vanessa Mdee moja ya tuzo mbili alizoshinda kupitia kibao alichomshirikisha cha Me and You kwa, tukio lililotafsiriwa kama ‘kumpoza’ binti huyo aliyeangukia pua katika kategori ya Msanii Bora Anayechipukia, ambayo ilienda kwa Ali Nipishe.
Bendi ya Mashujaa waliibuka kidedea zaidi katika mchakato huo, baada ya kujizolea tuzo tano, kupitia mbili za bendi (Wimbo Bora wa Bendi – Risasi Kidole) na Bendi Bora ya Mwaka, huku ikitwaa tatu za wasanii wake, ambao ni Chalz Baba aliyetwaa mbili za Mtunzi Bora wa Mashairi – Bendi na Msanii Bora wa Kiume – Bendi.
Pia rapa wake Ferguson aliibuka kidedea katika kategori ya Rappa Bora wa Bendi, alikowabwaga Greyson Semsekwa, J4, Jonico Flower na Sauti ya Radi.
Ukiondoa washindi wa Kategori 35, KTMA 2013 ilitoa tuzo mbili maalum; moja ya All of Fame ilitwaliwa na kundi la Kilimanjaro Band ‘Wana Njenje’ ambayo ilipokelewa na Waziri Ali, huku ile ya Individual All of Fame ikinyakuliwa na nyota wa muziki wa zamani marehemu Salum Abdallah na kupokelewa na mwanaye.
Hapa tunakuletea kategori zote 35 (washindi wakiwa katika wino mweusi – Italic), alama ya ‘tiki ikitangulia jina kuonesha kuwa ameshinda.
Wimbo Bora wa Mwaka
ü Dear God - Kala Jeremiah
Leka Dutigite - Kigoma All Star
Mapito - Mwasiti Feat Ally Nipishe
Me n U - Ommy Dimpoz Feat Vanessa Mdee
Pete- Ben Pol
Msanii Bora wa Kiume
Ben Pol
ü Diamond Platnumz
Linex
Mzee Yusuf
Ommy Dimpoz
Msanii Bora wa Kike
Isha Mashauzi
Khadija Kopa
ü Lady Jaydee ‘Comandoo’
Mwasiti
Recho
Msanii Bora wa Kike wa Taarab
ü Isha Mashauzi
Khadija Kopa
Khadija Yusuph
Leila Rashid
Msanii Bora wa Kiume wa Taarab
Ahmed Mgeni
Hashim Said
ü Mzee Yusuf
Msanii Bora wa Kiume Bongo Flava
Ally Kiba
Ben Pol
ü Diamond Platnumz
Linex
Ommy Dimpoz
Msanii Bora wa Kike Bongo Flava
Linah
Mwasiti
ü Recho
Shaa
Msanii Bora wa Hip Hop
Fid Q
Joh Makini
ü Kala Jeremiah
Profesa J
Stamina
Msanii Bora wa Kiume Bendi
ü Chalz Baba
Dogo Rama
Greyson Semsekwa
Jose Mara
Khaleed Chokoraa
Msanii Bora wa Kike Bendi
Anneth Kushaba
ü Luiza Mbutu
Mary Lucos
Vumilia
Msanii Bora Anayechipukia
ü Ali Nipishe
Angel
Bonge la Nyau
Mirror
Vanessa Mdee
Video Bora ya Mwaka
ü Baadae - Ommy Dimpoz
Kamili gado - Professor J Feat Marco Chali
Marry Me - Rich Mavoko
Nichum - Bob Junior
Party Zone - AY Feat Marco Chali
Mtunzi Bora wa Taarab
Ahmed Mgeni
Hemed Omary
Khadija Kopa
Mzee Yusuf
ü Thabit Abdul
Mtunzi Bora wa Bongo Flava
Ally Kiba
Barnaba
ü Ben Pol
Linex
Ommy Dimpoz
Mtunzi Bora wa Mashairi Hi Hop
Fid Q
Joh Makini
ü Kala Jeremiah
Mwana Fa
Stamina
Mtunzi Bora wa Mashairi Bendi
ü Chalz Baba
Grayson Semsekwa
Jonico Flower
Jose Mara
Khaleed Chokoraa
Mtayarishaji Bora wa Mwaka Bongo Flava
Bob Junior
Ima the boy
ü Man Water
Maneke
Marco chali
Mensen Selecta
Mtayarishaji wa Wimbo wa Mwaka Taarab
Bakunde
ü Enrico
Mtayaraishaji wa Wimbo wa Mwaka Bendi
Allan Mapigo
ü Amoroso
Mtayarisha Bora Anayechipukia
Imma the Boy
ü Mensen Selecta
Mr T Touch
Sheddy Clever
Rapa Bora wa Mwaka - Bendi
ü Fagasoni
Greyson Semsekwa
J4
Jonico Flower
Sauti ya Radi
Wimbo Bora wa Asili ya Kitanzania
Aambiwe - Offside Trick
Atatamani - AT
Boma la utete - Young D
ü Chocheeni kuni - Mrisho Mpoto Feat Ditto
Mdundiko - Momba Feat Juma Nature
Wimbo Bora wa Mwaka - Bendi
Chanzo ni sisi - Mapacha watatu
Jinamizi la Talaka - Mlimani Park Orchestra
ü Risasi kidole - Mashujaa band
Shamba la twanga - African Stars Band
Wimbo Bora wa Mwaka - Reggae
Hii si ya waoga - Yuzzo
ü Kilimanjaro - Warriors from The East
Natafuta Paradise - Mac Malick Simba
Salvation - Delayla Princess
Tunda - Hardmad
Wimbo Bora wa Afrika Mashariki
Fresh All Day - Camp Mulla
Make you dance - Keko Feat Madtrax
Maswali ya polisi - DNA
Still a Liar - Wahu
ü Valu Valu - Jose Chameleone
Wimbo Bora wa Mwaka Bongo Pop
Aifola - Linex Feat fundi Samweli
Baadae - Ommy Dimpoz Feat Angel
Chuki Bure - Sharo Milionea Feat Dully Sykes
Marry Me - Rich Mavoko
ü Me and you - Ommy Dimpoz Feat Vanessa Mdee
Wimbo Bora wa Ushirikiano
Chuki Bure - Sharo Millionea Feat Dully Sykes
Mapito - Mwasiti Feat Ally Nipishe
ü Me and U - Ommy Dimpoz Feat Vanessa Mdee
Sihitaji marafiki - Fid Q Feat Yvonne
Single Boy - Alikiba Feat Lady Jaydee
Wimbo Bora wa Hip Hop
Alisema - Stamina Feat Jux
Bum kubam - Nikki wa Pili Feat G Nako
Dear God - Kala Jeremiah
ü Nasema Nao - Nay wa Mitego
Sihitaji Marafiki - FID Q Feat Yvonne
Wimbo Bora wa Mwaka wa RnB
Amerudi - Belle 9
ü Kuwa na Subira - Rama Dee Feat Mapacha
Maneno maneno - Ben Pol
Pete - Ben Pol
Wimbo Bora wa Mwaka wa Ragga/Dancehall
Je ni nani - Ras Six
Muda upite - Susu Man
ü Predator - Dabo
Push Dem - Dr Jahson
Take it down - Chibwa and Tanah
Wimbo Bora wa Mwaka wa Taarab
ü Mjini chuo kikuu - Khadija Kopa
Mpenzi chocolate - Jahazi (Mzee Yusuph)
Si bure una mapungufu - Isha Mashauzi (Mashauzi Classic)
Sina muda huo - Jahazi (Leila Rashid)
Siwasujudii Viwavi jeshi -Isha Mashauzi (Mashauzi Classic)
Wimbo Bora wa Mwaka Zouk/Rhumba
Gubegube -Barnaba
Mapito - Mwasiti Feat Ally Nipishe
Nashukuru umerudi - Recho
ü Ni wewe - Amini
Sorry - Barnaba
Bendi Bora ya Mwaka
African Stars Band
Mapacha wa tatu
ü Mashujaa Band
Mlimani Park Orchestra (Sikinde)
Msondo Ngoma Music band
Kundi Bora la Mwaka la Taarab
Dar Modern Taarab
Five stars modern Taarab
ü Jahazi Modern Taarab
Kings modern Taarab
Mashauzi Classic
Kundi Bora la Mwaka Bongo Flava
ü Jambo squad
Makomando
Tip Top Connection
Tmk Wanaume Family
Weusi
No comments:
Post a Comment