MISIMU mitatu inabaki kuwa mingi kwa kiwango ambacho Jose Mourinho ameweza kudumu katika klabu kimoja. Mreno huyo amepita kwenye klabu za Chelsea, Benfica, Porto, Real Madrid, Inter Milan na Uniao de Leiria na hilo limetokea ndani ya miaka 13 tu.
Siku zote amekuwa ni mtu wa vipindi vifupi, na hiyo ndio sababu kubwa iliyowafanya wengi kuamini kwa nini hakupewa kazi ya kuinoa Manchester United baada ya kocha wake, Sir Alex Ferguson kutangaza kustaafu mwezi uliopita.
Ametwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya mara mbili, mataji manne ya ligi za ndani na tuzo nyingine zisizokuwa na idadi — hilo linaweza ugumu kuamini kwamba staili yake ya ufundishaji haifanyi kazi.
Alitangazwa kuwa kocha wa Chelsea wiki hii na uteuzi huo umefanywa kuwa tukio la siri kubwa kwenye historia ya soka duniani, huku mashabiki wa timu hiyo wakisubiri kwa hamu kuanza kwa msimu mpya wa 2013-14.
Kwa namna alivyoondoka kwenye klabu hiyo mwaka 2007, jambo hilo limesahaulika kabisa na Mourinho amejiandaa kuanza mwanzo mpya na bosi wake, Roman Abramovich.
Baada ya kuwa na staili ya kuhamahama kutoka klabu moja hadi nyingine, hatimaye sasa umefika wakati kwa kocha huyo, Mourinho kuweka mizizi sehemu moja na kuwa na utamaduni wa kudumu kwenye klabu moja.
Ni gwiji kwenye klabu ya Chelsea, shukrani kwa miaka yake mitatu ya mataji kede katika klabu hiyo ya Stamford Bridge. Hebu fikiria ingekuwa vipi kama angeamua kudumu mahali hapo kwa miaka sita?
Imekuwa si kazi rahisi kwa kocha kutoka kwingine kuingia kwenye Ligi Kuu England na kisha akafanikiwa kuweka utawala wake. United ilipoteza makali yake chini ya kocha Sir Alex Ferguson, Liverpool walifurahia nafasi yao waliyokuwa nayo wakati Mourinho alipowasili na Manchester City ilikuwa katika kipindi cha mpito.
Jose ataingia Stamford Bridge na kukutana na kikosi cha aina yake, kitu ambacho makocha wengi wa mchezo huo wa soka wangependa kukutana nacho.
Ni mabadiliko machache sana yanayohitajika kwenye kikosi hicho ili kukifanya kuwa na makali hatari zaidi na kuwa tishio duniani na Mourinho ni mtu mwafaka katika kulifanya hilo.
Akiwa kipenzi cha vyombo vya habari, akihusudiwa na mashabiki wa soka wa England; isingekuwa rahisi kwake kudumu Hispania, lakini maisha ya England yatakuwa mwafaka kwake.
Baadhi sababu ambazo zimekuwa zikimsababisha kushindwa kubaki kwenye timu moja muda mrefu ni kulumbana na wachezaji wake, bodi na watu wengine anaofanya nao kazi.
Habari nyingi zilielezwa kutokuelewa na ndugu yake Luis Lourenco, ndio chanzo kikubwa cha magumu yaliyomkabili kocha huyo alipokuwa Ureno.
Sifa yake kubwa ni kuwa na uwezo wa kujenga sifa zake, lakini tatizo kubwa linalomkabili ni kushindwa kuweka sawa mambo kwenye vyumba vya kubadilishia nguo, ndicho kitu kilichomharibia sifa zake huko alikotoka. Mfano halisi ni wachezaji Pepe na Iker Casillas.
Mou anaheshimika Stamford Bridge na hilo kamwe halitabadilika. Mashabiki wa Chelsea wanaamini atabadilika matendo yake na kukijenga kikosi hicho kuwa cha kiushindani zaidi na kutwaa mataji mfululizo kwa muongo mmoja au miwili mfululizo, kama alivyofanya Sir Alex katika kikosi cha United.
Hivyo kitu ambacho anapaswa kukifanya ili kumfanya afikie mafanikio kama ya Sir Alex ni kuachana na utamaduni wa kuhamahama na hivyo kuamua kutulia sehemu moja.
No comments:
Post a Comment