BEKI
wa Manchester United, Patrice Evra anajiandaa kutua Monaco.
Kocha
ajaye wa United, David Moyes anataka kutua na beki namba tatu wa Everton,
Leighton Baines, huku Evra akipata ushawishi mkubwa kutoka kwa mkewe anayemtaka
warudi kwao, Ufaransa.
Evra
alijiunga na United 2006 akitokea Monaco kwa pauni milioni 5.5.
Dzeko
chaguo la kwanza la Mourinho
KATIKA
orodha ya wachezaji Jose Mourinho anaotaka kuwasajili Chelsea majira haya ya
joto, Edin Dzeko ndiye chaguo lake la kwanza.
Hata
hivyo, Manchester City haitaki kumuuza mshambuliaji huyo kwa washindani wao wa
ubingwa wa England, lakini Mourinho anaamini atatumia mbinu mbadala kuweza
kumpata.
City
kama ilivyo kwa Chelsea, zote zinamhitaji Mshambuliaji wa Napoli, Edinson
Cavani ambaye anaelezwa kuwa na thamani ya pauni milioni 60, hivyo Mourinho
anaamini kama akilegeza uzi katika mbio hizo, basi anaweza kumnasa Dzeko.
Benteke
kupishana na Defoe Spurs
Tottenham inataka
kumtoa Jermain Defoe kwa Aston Villa sambamba na fedha, ili kuweza kummiliki
Mshambuliaji wao, Christian Benteke.
Klabu
hiyo ya Kaskazini mwa London inataka kufanya usajili huo wakushtukiza kwa
kumtoa kipenzi cha mashabiki wa England, Defoe.
Hivi
karibuni, Villa ilikataa kutoa nafasi ya kumsajili Defoe, 30, na badala yake
ikaelekeza nguvu zake katika kumpa Benteke mkataba wa muda mrefu zaidi.
Fernandinho
kumtangulia Pellegrini City
SIKU
ambayo Seville imetangaza dili la kumuuza winga wao, Jesus Navas kwa pauni
milioni 22 kwa Man City, Klabu hiyo ya England imethibitisha dili lingine la
kumsajili Kiungo wa Shakhtar Donetsk, Fernandinho, 28.
Klabu
hiyo ipo katika mazungumzo ya kununua mkataba wake ambao unaaminika kuwa na
thamani ya pauni milioni 15 na hivyo kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa kabla
hata Kocha mpya, Manuel Pellegrini hajatua Etihad.
Mourinho
amtaka Matic arudi Chelsea
KIUNGO
wa Benfica, Nemanja Matic ameendelea kuhusishwa na kurudi Chelsea.
Taarifa
zimeeleza kuwa, Jose Mourinho pia anataka kutua Chelsea na beki wa kushoto wa
Real Madrid, Fabio Coentrao, ambaye anaamini kwamba atawekwa sokoni.
Julai
2011, Real ililipa kiasi cha pauni milioni 25 kwa beki huyo mwenye miaka 25,
lakini inaaminika kuwa dau lake sasa ni pauni milioni 18.
Arsenal yatangaza dau la Sagna
Arsenal
inahitaji pauni milioni tano tu, ili kumwachia beki wake, Bacary Sagna.
Gazeti
la "The London Evening Standard", limeeleza kuwa Kocha Arsene Wenger
anataka suala la Sagna kuamuliwa haraka na kwamba atahitaji pauni milioni tano
tu.
Arsenal
imeendelea kumfukuzia Beki wa Borussia Dortmund, Lukasz Piszczek ili arithi
mikoba ya Sagna, lakini anaelezwa bado amebakiza miaka mitatu katika mkataba
wake na kwamba huenda zikahitajika pauni milioni 10 ili kuipata huduma yake.
Man Utd yamtega Strootman
KLABU ya Manchester United imeelekeza macho yake yote kwa Kiungo wa PSV Eindhoven, Kevin Strootman.
Gazeti
la "The Daily Mail", limeeleza kuwa United inataka kummiliki kiungo
huyo wa PSV Eindhoven anayeelezwa kuwa na thamani ya pauni milioni 25.
Kiungo
huyo wa Kimataifa wa Uholanzi, pia amekuwa katika rada za Everton msimu huu.
No comments:
Post a Comment