MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa
Cameroon na klabu ya Anzhi Makhachkala ya Urusi Samuel Eto’o ameteuliwa kuwa
mchezaji bora wa msimu wa Ligi Kuu ya nchi hiyo kwa msimu wa 2012-2013.
Eto’o
ambaye amewahi kunyakuwa tuzo ya mchezaji bora Afrika mara nne, alikabidhiwa
tuzo hiyo baada ya kuisadia timu yake kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye
msimamo wa ligi wan chi hiyo.
Akihojiwa mara baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo
Eto’o ambaye pia ni nahodha wa timu hiyo amedai kufurahishwa na hatua hiyo na
kuwashukuru mashabiki wa soka nchini humo pamoja na waandishi wa habari kwa kuwa
nyuma yake wakati wote.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 32 atakosa mchezo wa
kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2014 wa timu ya taifa ya nchi yake dhidi ya
Togo utakaochezwa Juni 9 mwaka huu kutokana na majeraha yanayomsumbua.
No comments:
Post a Comment