Kiungo Amri Ramadhani Kiemba amesaini mkataba wa miaka miwili na Simba leo mchana hivyo ataendelea kuichezea klabu
hiyo kwa msimu ujao
Akizungumza na Lenzi ya Michezo jioni hii Kaimu Mwenyekiti
wa Simba, Joseph Itang’are ‘Mzee Kinesi’ alisema ni kweli wameshaingia mkataba
na mchezaji huyo leo mchana.
Pia nilizungumza na Kiemba wakati akiwa kwenye mazoezi ya
timu ya taifa na kukiri kuingia mkataba wa miaka miwili hivyo ataendelea kuwepo
Msimbazi
“Mimi kweli nimesaini Simba ila nashangaa magazeti yalikuwa
yanatoa wapi habari za mimi kuwa nimesaini Yanga kwani sikuwahi kuongea nayo”,
alihoji Kiemba.
Kiemba kwa sasa yupo kambini na timu ya Taifa kujiandaa na mchezo
na Ivory Coast utakaochezwa jumapili hii
baada ya mchezo uliopita kufungwa na Morocco mabao 2-1, bao ambalo stars
ililipata kupitia kwa Amri Kiemba dakika ya 62.
No comments:
Post a Comment