MCHEZAJI wa kimataifa wa Uganda Cranes, Musa Oloya huenda
akatua Simba Sports Club kwa msimu ujao kwa mkataba wa miaka miwili.
Simba ambayo ilivuliwa ubingwa msimu wa 2012/13 sasa inajiandaa kwa mashindano ya Kombe
la Kagame (CECAFA) iliyopangwa kufanyika
Sudan mwezi ujao.
Timu hii pia inajengwa
upya kwa ajili ya msimu ujao na kuzipa pengo la wachezaji waliondoka kama winga Mrisho Ngassa ambaye
amejiunga mabingwa wa Ligi kuu ya Tanzania , Yanga.
mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba, Zacharia Hanspoppe
alithibitisha majadiliano yapo hatua ya juu na nyota wa Uganda ambaye yupo
katika kikosi cha Uganda Cranes.
Oloya, ambaye zamani alikuwahi kuchezea Saigon Thanh Xuan wa
Vietnam, anatarajiwa kujiunga na Simba ya Tanzania baada ya Cranes kucheza mchezo
wa kirafiki na Libya na wa kufuzu Kombe
la Dunia 2014 mwezi ujao.
Oloya atajiunga na
mwenzake toka Uganda Samweli Ssekoom ambaye alikuwa mchezaji wa Mamlaka ya
Mapato Uganda (URA) ambaye amesaini Simba maarufu kama Msimbazi Street.
Simba hadi sasa ina wachezaji wa tano kigeni, ambao ni pamoja
na Kipa Abel Dhaira na Mude Mussa (Uganda), Felix Sunzu (Zambia)
Simba pia imewasajili beki Issa Rashid,(baba Ubaya) mlinzi Andrew Ntalla, mshambuliaji Zahor Pazi
na kiungo Twaha Shekuwe.
Simba ilishika nafasi ya tatu katika msimu uliomalizika
2012/13 nyuma ya Yanga FC washindi na nafasi ya
pili ilichukuliwa na Azam.
No comments:
Post a Comment