Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, May 22, 2013

MRISHO NGASSA AZUA JAMBO TFF, SIMBA WAAMBIWA WAWE WAVUMILIVU KIPINDI CHA USAJILI KITAFIKA





Katika hali isiyokuwa ya kutegemewa kuhusu simtofamhamu wa uhalali wa mshambuliaji Mrisho Ngassa aliyejiunga na Simba akitokea Azam FC kwa mkopo na kukubaliana na uongozi wa Yanga hivi karibuni, Mwenyekiti wa kamati ya usajili wa timu hiyo ya Simba  Zakaria Hans Pope amesema kuwa klabu ya Yanga inajisumbua kumsainisha mchezaji   huyo amewaeleza wasahau.

Hans Pope ameyasema hayo kwa  njia ya simu, kuwa Ngasa bado ana mkataba wa mwaka mmoja zaidi wa kuitumikia klabu ya Simba ambao aliusaini yeye mwenyewe.

Pia amesema sehemu pekee ya kujua uhalali wa mkataba huo ni kwenye ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ambapo ilipelekwa kwa ajili ya kumbukumbu zaidi.

Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura amesema uhalali wa mchezaji hupnutatolewa ufafanuzi kipindi cha usajili kitakapo fika na kuitaka Simba wawe wavumilivu kwani kwa sasa hakuna usajili uliowasilishwa TFF.

Wakati Ngassa anatambulishwa Yanga alisema anafurahi kurudi kwenye timu anayoipenda   pia alipoulizwa kuhusu mkataba na Simba alikana kuwa na mkataba na timu hiyo kwani lile gari aina ya Verosa na pesa waliyompa ilikuwa ni kumshawishi ili ajiunge na timu hiyo na si vinginevyo.

No comments:

Post a Comment