MCHEKESHAJI wa Kundi la Original Comedy ambaye pia ni msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Mujuni Sylivester ‘Mpoki’, anatarajia kuachia ngoma yake mpya hivi karibuni inayokwenda kwa jina la ‘Mademu’.
Mpoki alisema katika ngoma hiyo,
amezungumzia utofauti uliopo kati wanawake wa uswailini na wale wanaoishi kwenye
familia bora.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mpoki alisema ameangalia suala la elimu amegundua kuna utofauti mkubwa wa kozi wanazochagua wasichana walio kwenye familia bora na wale wanaotoka kwenye familia maskini.
“Wasichana waliozaliwa kwenye familia bora huchagua kusoma kozi za gharama kama ‘Air Ticketing’ na zingine ambazo ada yake ni kubwa wakati wale maskini huishia kusoma kozi kama za ualimu kwakuwa ndizo wanazomudu kuzilipia,” alisema.
Mpoki alisema utofauti huo ndio unaoleta matabaka makubwa kati ya wale walionazo na wasiokuwa nazo.
Ameongeza kuwa japokuwa katika nyimbo zake hutumia maneno ya utani, lakini lengo lake ni kufikisha ujumbe kwa serikali ili ikumbuke kuwajibika zaidi na kuwajali wananchi wake wanaoishi maisha magumu.

No comments:
Post a Comment