Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Rwanda Milutin “Micho” Sredojević amechaguliwa kuwa mkufunzi mpya wa timu ya taifa ya Uganda akiziba nafasi ya Bobby Williamson ambaye aliachishwa kazi mwezi jana
Micho ambaye ni raia wa Serbia amechaguliwa jana katika makao makuu ya Shirikisho la soka la Uganda (Fufa House) huko Mengo, kilometa chache kutoka jiji la Kampala na ametia saini kandarasi ya miaka miwili .
Williamson aliiongoza Uganda Cranes kushinda mara nne kombe la baraza la vyama vya soka la Afrika Mashariki na Kati Challenge Cup lakini alishindwa kuipeleka ti mu hiyo katika mashindano ya mataifa ya afrika .
Aidha Micho amesema na akitumia Lugha ya kiganda kwa lafudhi mbaya " Luganda , “Nasikia heshima sana na kujivunia kupewa kuifundisha timu ya taifa ya Uganda ambayo aliiondoka Uganda 2004, nilikuwa sipo kimwili lakini roho yangu ilikuwa hapa na inapendeza sana kurudi hapa. Na nina imani kuipeleka nchi mbali zaidi ”
Micho, 43, atasaidiwa na kocha wa timu ya polisi ya uganda Sam Timbe, na kocha wa Bul Bidco Kefa Kisala na kipa wa makocha Fred Kajoba.
Aidha kocha huyo amewahi kufundisha timu za St.George of Ethiopia, South Africa’s Orlando Pirates pia Al Hilal ya Sudan
No comments:
Post a Comment