Manchester City jana walimaliza msimu wakiendelea kuumia baada ya kuchabangwa mabao 3-2 wakiwa kwao nyumbani Etihad wakiongozwa na Viongozi wa muda baada ya kumtimua kocha wao Roberto Mancini wiki iliyopita.Leo imekuwa wiki ya kasheshe pia baada ya funga nikufunge ya Norwichi City kuwafungia msimu kwa kuwaadabisha bila huruma nyumbani kwao. Mabingwa hawa waliovuliwa ubingwa na Manchester United msimu huu baada ya kushindwa kujitetea mabao yao ya leo yamefungwa na mchezaji Jack Rodwell yote mawili dakika ya 29 na kipindi cha pili dakika ya 59.City wanaambulia patupu msimu huu baada ya kosa kombe lolote na hivi karibuni walifungwa na Wigan inayoshuka daraja msimu huu wakiwa na kombe na kwa historia yakipekee kushuka daraja msimu huo huo. Bao za Noerwich City zimefungwa na Pilkington dakika ya 26, Holt dakika ya 54 na la mwisho na ushindi akalifunga Howson dakika ya 65. City wanaoshikilia nafasi ya pili kwenye msimamo watacheza uefa Champions League kwenye makundi.
Joe Hart akiangalia mpira unavyoishilia nyavuni uliopigwa na Holt
Holt hakuweza kujinyima nafasi ya kushangilia bao lake
Carlos Tevez alitolewa na kuingia Sergio Aguero kipindi cha pili.
Rodwell akifunga bao la pili
Anaitwa Jonny Howson ndiye aliyefunga bao jingine
Kipa wa City Joe Hart Hoiii...
Hoi...nyumba yao imechomwa City
Msimu umeisha salamu za mwisho...tutaonana tena kwenye mechi za mazoezi
Viongozi wa Norwich wakipunga mikono yao juu baada ya kazi nzuri ya kumfunga City bao 3-2
VIKOSI:
Manchester City: Hart, Richards, Zabaleta, Lescott, Kolarov, Milner, Nasri, Rodwell (Silva, 65), Y Toure, Dzeko, Tevez (Aguero, 50)
Subs not used: Pantilimon, Maicon, Clichy, Garcia, Barry
Goals: Rodwell 29, 59
Norwich: Ruddy, Martin, Whittaker, Garrido,
R Bennett, Johnson (Tettey, 65) Snodgrass, Howson, Pilkington (E Bennett, 81), Hoolahan, Holt (Becchio, 90)
Subs not used: Bunn, Barnett, Fox, Butterfield
Goals: Pilkington 26. Holt 54, Howson 65
Ref: Mark Halsey
Att: 47,054
MATOKEO YA MECHI ZOTE ZA LEO.
Jumapili 19 Mei
Chelsea 2 Everton 1
Liverpool 1 QPR 0
Man City 2 Norwich 3
Newcastle 0 Arsenal 1
Southampton 1 Stoke 1
Swansea 0 Fulham 3
Tottenham 1 Sunderland 0
West Brom 5 Man United 5
West Ham 4 Reading 2
Wigan 2 Aston Villa 2
No comments:
Post a Comment