
Mshambuliaji Queens Park Rangers Loic Remy amekamatwa kwa makosa ya ubakaji na wenzake wawili.
Mshambuliaji huyo mwenye miaka 26 ambaye pia ni mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa anashikiliwa na askari wa uchunguzi wa Scotland Yard's wa kitengo cha makosa ya ubakaji akiwa pamoja na vijana wenzake wawili ambao walikamatwa huko Fulham, Magharibi mwa London .
Vijana hao wanashikiliwa kwa mahojiano zaidi baada ya kumuingilia mwanamama mwenye miaka 34 ambaye alibakwa siku ya jumatatu na mashitaka hayo yalipitiwa na Met kutoka Askari wa Kent jumatatu iliyopita.
Msemaji wa Metropolitan Polisi amesema : "watu watatu wenye umri kati, miaka 26, 23 na 22, walikamtwa katika kitongoji cha Fulham kwa makosa ya ubakaji na bado watabakia katika kituo cha polisi hapa London ".
No comments:
Post a Comment