Mudathir akiwa na mpira wakati wa mazoezi ya stars |
KIUNGO kinda
mshambuliaji wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ Mudathir Yahya jana alionekana
kuwafunika washambuliaji Mrisho Ngasa na Salum Abubakar kwenye mazoezi ya timu
hiyo yanayofanyika Uwanja wa Karume.
Mudathir
Yahya anayetokea Azam FC alionekana kumfurahisha kocha Kim Poulsen kutokana na
uwezo wake wa kufuatilia mafundisho yake kwa vitendo walipokuwa kwenye mazoezi
ya timu hiyo.
Mudathir
ambaye ni mara yake ya kwanza kuitwa kwenye kikosi cha wakubwa, awali alikuwa
kwenye timu ya vijana waliochini ya miaka 17 ‘Serengeti boys’, kocha alimwita
kwenye stars ndogo na kuweza lkufanya vizuri na sasa yupo kwenye timu ya
wakubwa ambako pia ameonyesha kuwa anaweza.
Kijana huyu
ambaye ni mpole na siyo muongeji kutokana na jinsi alivyokuwa anacheza
alijikuta akishangiliwa na mashabiki waliokuwepo uwanjani kushuhudia mazoezi
hayo.
Alisikika
shabiki akisema ‘Serengeti boys huyu atawanyang’anya namba mafadha sasa hivi
maana yupo fiti na kocha anamkubali pia’.
Taifa stars
ipo kambini kujiandaa na mchezo dhidi ya Morocco lakini pia kabla ya kurudiana
na Morocco utakaochezwa Juni 8, mwaka huu lakini itacheza mchezo wa kirafiki na Sudan, wakati
wakiwa safari kwenda Morocco mchezo utakaochezwa nchini Ethiopia Juni 2, mwaka
huu
Meneja wa
Timu hiyo Taso Mukebezi alisema wachezaji wote wapo kambini na wana afya njema
isipokuwa Mwinyi Kazimoto ana jereha dogo kwenye mguu ambalo lilitokana na
kuchubuka wakati wa mazoezi ya asubuhi.
“Timu
imekamilika isipokuwa Mwinyi Kazimoto amepumzika kwani asubuhi alipata mchubuko
kwenye mguu na wachezaji Thomas Ulimwengu na Mbwana Samata wataungana na timu
Morocco wakitokea Congo”, alisema Mukebezi
Pia timu inaendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Karume leo asubuhi na jioni hadi
Mei 26, mwaka huu.
No comments:
Post a Comment