Mancin |
Pellegrini |
BAADA ya jana Manchester City kupata kipigo toka kwa Wigan kwenye mchezo wa kombe la FA
Robert Mancini ametimuliwa kibarua chake
Mancini pamoja na kuwa alisaidia City kutwaa Ubingwa wa Ligi
Kuu ya Uingereza, Kombe la FA na kushika nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu ya England
msimu huu imevuliwa makombe yote msimu huu na uliopita.
Nafasi ya Mancini huenda ikachukuliwa na Pellegrin kwani uongozi
wa City inasemekana ulikutana na wakala wake wiki mbili zilizopita na uongozi
wa City haukuonyesha juhudi za kukanusha kwamba ulikutana na wakala wa
Pellegrin na aliyefanya naye mazungumzo ni Txiki.
Taarifa za Txiki kukutana na wakala wa Pellegrini zilianza
kuchukua nafasi tokea wiki iliyopita na uongozi wa City ulionekana kuwa kimya
kabisa kuhusiana na suala hilo.
Bado haijajulikana rasmi ataondoka leo usiku, kesho au
keshokutwa lakini inaonekana hakuna uhakika kama atakuwepo kwenye benchi kesho
wakati City watakapokuwa wakiivaa Reading.
Habari za uhakika kutoka ndani ya Man City zinaeleza, uamuzi
wa kumtimua Mancini ulichukuliwa katika kikao cha pamoja kilichowajumuisha
mabosi wawili Ferran Soriano, Txiki Begiristain na Mwenyekiti wa klabu hiyo,
Khaldoon Al Mubarak ikiwa ni siku moja tu baada ya City kuchapwa bao 1-0 katika
mechi ya fainali ya Kombe la FA.
The Sun la Uingereza lilifanya juhudi za kumnasa Mancini ili
azungumzie suala hilo lakini haikuwezekana lakini kumekuwa na taarifa amebanwa
kwa kuwa anashughulikia suala la malipo ya fedha zake baada ya mkataba wake
kusitishwa.
Ingawa yeye alisema
jana amebakiza miaka minne na City, lakini taarifa zinaeleza ana miaka mitatu
iliyosalia na alisaini baada ya kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu England.
No comments:
Post a Comment