KOCHA Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts amesema ubora wa Uwanja
wa Gombani uliowekwa nyasi bandia utawapa matokeo mazuri katika mechi yao dhidi
ya Simba.
Kutokana na mazoezi wanayofanya kwenye uwanja huo, ni wazi
Simba imekwisha habari yake ambao watacheza Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Brandts alisema amevutiwa na miundombinu ya
uwanja huo, hivyo itakuwa ni fursa kwa wachezaji wake kuhitimisha msimu wa ligi
hiyo kwa kuibuka na ushindi.
Brandts alisema ana matumaini makubwa Yanga itaibuka na
ushindi, ili waweze kulinda heshima
baada ya kuchukua ubingwa wa ligi hiyo.
Alisema wamefurahi kuona timu yake ikifanya mazoezi katika
uwanja ulio bora, kitu ambacho ataweza kuijenga timu yake vizuri kabla ya
kukutana na watani wao wa jadi Simba.
Brandts alisema kazi iliyobaki ni kuhakikisha wachezaji wake
anawapa mbinu mbalimbali zitakazoweza kuwapatia ushindi.
Yanga ilianza kufanya mazoezi kwenye uwanja huo juzi, baada
ya kutua katika kisiwa hicho Ijumaa wiki iliyopita.
Uongozi wa klabu ya Yanga kwa kushirikiana na benchi la
ufundi, uliamua kubadilisha mazingira ya kambi ambao walikuwa na mazoea ya
kwenda Bagamoyo.
Wakati huo huo, Brandts alisema wachezaji wake wapo fiti
kiakili, kifikra na morali ya hali ya juu kuelekea mechi hiyo.
No comments:
Post a Comment