Kikosi cha Yanga |
Kikosi cha JKT Oljoro |
Hamis Kiiza akipambana na beki wa JKT Oljoro |
Nadir Haroub akikimbia baada ya kufunga bao la kwanza huku wachezaji wenzake wakimkimbilia |
Beki wa JKT Oljoro Shaibu Nayopa akiondosha mpira eneo la hatari |
TIMU ya Yanga leo imejikita kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Barabaada ya kuifunga JKT Oljoro mabao 3-0 kwenye mchezo uliochezwa
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Yanga imetimiza pointi 52 baada ya kucheza mechi 22,
ikifuatiwa na Azam yenye pointi 46, ambayo keshoitakuwa na kibarua cha
kujiuliza kwa Simba zile bao 3-0 kwenye raundi ya kwanza zilikuwa halali
Hamisi Kiiza alipokea pasi nzuri ya Niyonzima na kumpiga chenga
chenga kipa wa JKT kabla ya kuusukuma mpira nyavuni na bao la tatu dakika ya
43.
Bao la kwanza lilitiwa kimiani na Nadir Haroub ‘Cannavaro’
kwa kichwa baada ya mpira wa kona aliyopiga Haruna Niyonzima na kuokolewa na
nahodha wa JKT Oljoro Shaibu Nayopa na kutua kichwani mwa Nadir Haroub na
kuuzamisha kirahisi wavuni.
Simon Msuva alifunga bao la pili kwa shuti la mbali nje ya
eneo la penalty alipokea pasi maridadi
ya David Luhende mabeki wa JKT Oljoro dakika ya 16
Mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda Hamis Kiiza alifunga bao
la tatu baada ya kuwatoka mabeki wa JKT Oljoro na kumalizia na kumpiga chenga
kipa na kufunga bao dakika ya 43 pia mchezaji Juma Abdul aliumia na kutolewa na
nafasi yake kuchukuliwa na Shadrack Nsajigwa.
Kipindi cha pili, baada ya dakika mbili tu Oljoro ilipata
pigo baada ya kipa wake Mussa Lucheke kuumia na kumpisha Shaibu Issi na alipoingia kipa huyu Yanga walikosa mabao mengi ya wazi kwenye
mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi Amon Paul toka Mara akisaidiwa na John
Kanyenye wa Mbeya na Arnord Bugado wa Singida.
Kikosi cha Yanga ni; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul,
David Luhende, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’,
Simon Msuva, Frank Domayo, Hamisi Kiiza, Didier Kavumbangu na Haruna Niyonzima.
JKT Oljoro; Mussa Lucheke, Yussuf Machogoti, Majaliwa Sadik, Nurdin Mohamed,
Shaibu Nayopa, Salim Mbonde, Karage Mgunda, Emmanuel Memba, Paul Nonga, Iddi
Saleh na Hamisi Saleh.
Huko Mbeya Tanzania Prison yaifunga JKT Ruvu mabao 2-0 kwenye mchezo wa ligi Kuu uliochezwa uwanja wa Sokoine.
Ushindi huu umechagizwa na mashabiki wa soka wa mkoa huo kuanza kuichangia timu hiyo ili isishuke daraja wakiongozwa na Naibu Waziri wa Elimu, Mh. Mwilugo
Huko Mbeya Tanzania Prison yaifunga JKT Ruvu mabao 2-0 kwenye mchezo wa ligi Kuu uliochezwa uwanja wa Sokoine.
Ushindi huu umechagizwa na mashabiki wa soka wa mkoa huo kuanza kuichangia timu hiyo ili isishuke daraja wakiongozwa na Naibu Waziri wa Elimu, Mh. Mwilugo
No comments:
Post a Comment