Shaban Dihile wa JKT Ruvuakidaka mpira kichwani mwa Mbuyu Twite wa Yanga
YANGA leo
imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JKT Ruvu kwenye mchezo wa Ligi Kuu
Tanzania Bara uliochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kwa matokeo
hayo Yanga imetimiza pointi 56 na sasa inahitaji pointi moja tu ili kutawazwa
mabingwa baada ya kuwa Simba imeshautema rasmi.
Bao la
kwanza lilifungwa na Simon Msuva baada ya kupokea mpira wa kurusha uliorushwa
na Mbuyi Twite.
Kipindi cha
pili, Yanga SC walirudi wakiwa wanadhamira ya kuongeza mabao zaidi na
kufanikiwa kupata mabao mawili zaidi, yaliyofungwa na Hamisi Kiiza dakika ya 59
na Nizar Khalfan dakika ya 64.
Kiiza
alifunga kwa kichwa akiunganisha mpira wa adhabu uliopigwa na David Luhende,
baada ya Nizar Khalfan kuchezewa rafu nje kidogo ya eneo la hatari.
Nizar yeye
alifunga baada ya kuuwahi mpira uliogonga mwamba na kurudi baada ya Frank
Domayo kuunganisha krosi ya Haruna Niyonzima.
Kikosi cha
Yanga SC kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’/Said Mohamed dk 86, Mbuyu Twite,
David Luhende, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’,
Frank Domayo, Haruna Niyonzima, Nizar Khalfan/Said Bahanuzi dk90, Hamisi
Kiiza/Jerry Tegete dk82 na Simon Msuva.
JKT Ruvu; Shaaban Dihile, Hassan Kikutwa/Sostenes Manyasi
dk77, Stanley Nkomola, Ramadhani Madenge, Damas Makwaya, Nashon Naftali, Amos
Mgisa, Ally Mkanga/Charles Thadei dk78, Mussa Mgosi, Zahor Pazi na Haroun
Adolph.
|
No comments:
Post a Comment