AZAM FC leo imetoka sare ya bila kufungana na AS FAR Rabat
ya Morocco katika mchezo Kombe la Shirikisho Afrika uliochezwa Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam.
Matokeo hayo yanaifanya Azam iwe na mtihani mgumu katika
mchezo wa marudiano wiki mbili zijazo Morocco, wakitakiwa lazima kushinda au
kutoa sare ya mabao ili kufuzu.
Pamoja na sare hiyo, Azam watakumbuka sana mabao matatu ya
wazi waliyokosa kupitia kwa washambuliaji wao wa pembeni, Kipre Herman Tchetche
mawili na Khamis Mcha ‘Vialli’ moja,
Kipre aligongesha mwamba mashuti mawili katika dakika za 51
pembeni kushoto katikati na dakika ya
90+1 mwamba wa juu katikati baada ya jitihada za kuwatoka mabeki wa AS FAR
Rabat.
Khamis Mcha naye alimtoka vizuri beki wa pembeni wa AS FAR
Rabat dakika ya 52 lakini akapiga nje shuti lake.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi Emile Fred wa Shelisheli,
akisaidiwa Steve Maire na Jean Ernesta huku mezani akiwepo Jean Claude Labrosse
wote wakitokea nchini Shelisheli.
Lakini kipindi cha pili, walifunguka na kuanza kushambulia
moja kwa moja jambo ambalo liliweka kwenye misukosuko lango la AS FAR Rabat kwa
muda mrefu hadi wachezaji wa timu hiyo kuanza kufanya hila za kupoteza muda ili
kupunguza kasi ya wenyeji.
John Raphael Bocco ‘Adebayor’ naye alilitia misukosuko mara
kadhaa lango la wageni kila ilipoingizwa mipira ya juu kutokea pembeni hususan
kona japokuwa alikuwa chini ya ulinzi mkali leo.
Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Mwadini Ally, Himid Mao, Waziri
Salum, David Mwantika, Joackins Atudo/Luckson Kakolaki dk7, Kipre Balou, Kipre
Tchetche, Salum Abubakar, John Bocco ‘Adebayor’, Humphrey Mieno na Kahmis Mcha
‘Vialli’/Mwaikimba dk78.
AS FAR Rabat; Ali Grouni, Mustafa Mrani, Younes Hammal,
Younes Belakhdar, Yassine El Kordy, Abdelrahim Achchakir/Mostafa El yousfi
dk74, Salaheddine Said, Mohamed El Bakkali, Salaheddine Aqqal/Souffiane Alloudi
dk80, Mustafa Allaoui na Hicham El Fathi/Youssef Anouar dk 69.
No comments:
Post a Comment