SHIRIKISHO la Soka barani Ulaya-UEFA limepanga kuanzisha adhabu mpya kali ya kupambana na ubaguzi wa rangi ambapo wachezaji watakaokutwa na hatia ya kufanya vitendo hivyo watafungiwa si chini mechi 10.
Katibu Mkuu wa UEFA Gianni Infantino amesema pia watafunga viwanja kwa muda viwanja ambavyo mashabiki wake watafanya tukio kama hilo kwa mara ya kwanza na kuufunga kabisa kama mashabiki wa timu husika watarudia tukio hilo kwa mara ya pili pamoja na faini ya fedha nyingi. Adhabu hizo mpya ambazo zilizungumziwa katika kikao cha kamati ya utendaji ya UEFA kilichokutana jana kitahusisha mechi zote za mashindano barani Ulaya.Infantino alifafanua kuwa kama mashabiki wa klabu fulani watakutwa na hatia ya kufanya vitendo hivyo basi upande wa uwanja uliohusika na tukio hilo utafungwa lakini kama tatizo ilikijirudia basi mashabiki wote watazuiwa kuingia uwanjani na kutozwa faini itakayofikia dola 65,300.
No comments:
Post a Comment