TIMU ya
soka ya waandishi wa habari za Michezo nchini (Taswa FC) na timu ya netboli
(Taswa Queens) itaondoka jijini Jumatano alfajiri kwenda Kibiti,
mkoa wa Pwani kwa ajili ya mechi maalum ya kirafiki.
Mechi hiyo imepangwa kufanyika kwenye uwanja wa Samora imeandaliwa kwa ajili ya kuanzisha uhusiano wa karibu baina ya waandishi wa habari za michezo na walimu wa wilaya hiyo katika kuendeleza sekta hiyo hapa nchini.
Mwenyekiti wa Taswa FC, Majuto Omary alisema kuwa mechi ya kwanza siku hiyo itakuwa kati ya Taswa Queens na kombaini ya walimu iliyopangwa kuanza saa 9.00 ambapo mechi ya pili itakuwa kati ya Taswa FC na kombaini ya walimu iliyopangwa kuanza saa 10.00 jioni.
Majuto
alisema kuwa mbali ya kuanzisha uhusiano na kupromoti michezo katika wilaya
hiyo, mechi hizo pia zitakuwa sehemu ya maandalizi ya Taswa FC na Taswa Queens
kwa ajili ya ziara ya kimichezo mkoani Arusha na Tanga mwezi ujao.
“Maandalizi
ya safari yamekamilika na tunawaomba wachezaji wazingatie muda wa kufika ili
tuweze kuondoka kwa mujibu wa ratiba yetu, lengo ni kuwahi kufika na kumaliza
mapema na kuendelea na ratiba nyingine kwa mujibu wa wenyeji wetu,” alisema
Majuto.
Alisema
kuwa timu zao zote zimejiandaa kwa ushindi katika mechi hizo ambazo
zinatarajiwa kuwa na ushindani mkali kutokana na maandalizi. Taswa FC
haijapoteza hata mechi moja toka kuanza kwa mwaka huu. Timu zote mbili zilitoa
vipigo kwa timu ya Kiliflora ya Arusha kwa mabao 4-1 kwa upande wa soka na
mabao 28-8 kwa upande wa netiboli.
Mratibu
wa mechi hiyo, mwalimu Paul Nyoni amesema kuwa maandalizi yote yamekamilika na
wanawasubiri kwa hamu waandishi wa habari. Nyoni alisema kuwa wamewaandaa
mapokezi mazuri kwa waandishi na wanaamini mechi hizo mbili.
No comments:
Post a Comment