Nadal kushoto akitoa neno la shukrani kwa waliohudhuria fainali hiyo, huku Djokovic akitabasamu akiwa na kombe la ubingwa wa Monte Carlo Masters 2013.
MONACO, Ufaransa
"Sikujua kama naenda kuwa sehemu ya mafanikio ya michuano hii mwaka huu. niliamua kukubali kucheza mashindano haya, na hivi sasa najiona kwamba nilifanya maamuzi sahihi mno katika maisha yangu ya michezo"
KINARA wa ubora katiika viwango vya dunia vya mchezo wa tenisi, Novak Djokovic juzi alihitimisha mfululizo wa miaka minane wa nyota Rafael Nadal kushinda michuano ya Monte Carlo Masters, kwa kumchapa na kutwaa ubingwa huo katika fainali.
Djokovic nyota wa kimataifa wa Serbia, amempa kichapo cha kwanza Nadal katika michuano ya Monte Carlo katika mechi 47, akilipa kisasi cha mwaka jana alipoangukia pua katika fainali ya michuano ya Masters.
Nadal alishuhudia Djokovic, 25, akianza kwa kaaasi na kushinda seti ya kwanza kwa 6-2 katika muda wa dakika 46, kabla ya kushinda 7-6 na kulala 7-1 katika seti ya mwisho.
Djokovic alikuwa akihaha kutokana na jeraha la enka lililokuwa likimsumbua tangu raundi ya awali, lakini hakuonesha dalili za kukwazwa na hali hiyo mchezoni na kupigana kuweza kumshinda hasimu wake huyo.
"Sikujua kama naenda kuwa sehemu ya mafanikio ya michuano hii mwaka huu. niliamua kukubali kucheza mashindano haya, na hivi sasa najiona kwamba nilifanya maamuzi sahihi mno katika maisha yangu ya michezo," alisema Djokovic.
Katika mechi hiyo ya kwanza baina yao tangu Nadal aliposhinda fainali ya French Open Juni mwaka jana, Djokovic alielemewa katiika seti ya kwanza akiwa nyuma kwa 5-0, huku Nadal akitisha na kuaminisha wengi kuwa angeshinda fainali hiyo.
BBC Sport
No comments:
Post a Comment