Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, April 5, 2013

SITA BORA YA SOKA CHAMA CHA MKOA WA DAR ES SALAAM (DRFA) KUANZA APRILI 9 MWAKA HUU


CHAMA cha Soka Dar es Salaam (DRFA), kimetangaza kuanza kwa Ligi Daraja la Pili Mkoa wa Dar es Salaam, hatua ya sita bora itakayochezwa kwenye viwanja vitatu.
Akizungumza na waandishi wa Habari, Ofisa Habari wa DRFA, Mohamed Mharizo, amesema kuwa ligi hiyo itaanza Aprili 9, mwaka huu hadi 31 katika viwanja vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Kinesi na Makurumla.
Alizitaja timu zitakazochuana katika hatua hiyo kuwania kucheza Ligi ya Kanda kuwa ni pamoja na Boom FC ya Ilala, Friends Rangers ya Magomeni, Abajalo FC ya Sinza, Red Coast ya Mburahati, Day Break ya Magomeni na Shariff Star ya Ilala.
“Kwa mujibu wa ratiba yetu, kila siku kutakuwa na mechi tatu, hivyo katika mechi za ufunguzi Aprili 9, Boom FC wao watachuana na Shariff Star, kwenye Uwanja wa Airwing, wakati Day Break watamenyana na Friends Rangers uwanja wa Makurumla huku Red Coast wao watacheza dhidi ya Abajalo,” alisema Mharizo.
Timu tatu katika ligi hiyo zitawakilisha mkoa katika Ligi ya Kanda.
Wakati huo huo, Mharizo amesema kabla ya kuanza kwa ligi, kutatolewa semina elekezi kwa viongzi wa timu shiriki, itakayofanyika jumapili kwenye Ukumbi wa Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa iliyopo Ilala kuanzia saa nne asubuhi.
“Lengo la semina hii ni kutoa elimu kwa viongozi na wachezaji ili kuondoa mvutano wakati wa ligi hiyo kwani nia yetu tunapenda kuona ligi ikichezwa kwa kufuata kanuni na taratibu zilizowekwa,” alisema Mharizo.
Semina hiyo itawahusisha viongozi wa timu ambao ni  makatibu, wenyeviti, makocha, Nahodha na Waamuzi 16 watakaochezesha ligi hiyo.

No comments:

Post a Comment