Di Canio akitoa maelekezo kwa Adam Johnson |
LONDON, England
MASHABIKI wa Sunderland walisimama na kuwasifia mashujaa wao baada ya ushindi dhidi ya Everton. Baadhi walipiga makofi, wengine walishangilia na wengine walipiga kelele za furaha.
Lakini, sauti iliyokuwa hapa ni ile ya kuliimba jina la Paolo Di Canio kuliko muziki uliokuwa ukisika kutoka kwenye spika zilizopo kwenye uwanjani hapo. Wote walimsifu Paolo Di Canio, mtawala mpya wa Sunderland.
Lilikuwa ni tukio la sanaa ya aina yake, ilikuwa burudani safi na Di Canio, amekuwa kipenzi cha watu kwenye timu hiyo, anaheshimika na anayewafanya kujiona wasiofanya kosa kwa kuichagua Black Cats.
Kabla ya kutoka uwanjani hapo baada ya filimbi ya mwisho, alisimama kwa mara nyingine, alitembea ndani ya uwanja na kuwaonyesha mashabiki waliokuwa jukwaani tena kwa kusisitiza nguvu alizonazo kwa kukaza misuli ya mikono yake kuonyesha ubavu wake.
Baada ya mechi tatu tu, Di Canio anapepea. Ameiteka klabu hiyo na jiji kwa ujumla. Kama kulikuwa na mpinzani katika uteuzi wake pengine kutokana na sababu za kisiasa, kwasababu atakuwa amechukulia jambo hilo tofauti na bila shaka ataanza kumhusudu kocha huyo kutokana na hali inavyoendelea kwa sasa.
Baada ya kuwafunga wapinzani wao wa mji mmoja, Newcastle United katika mechi yake ya pili tangu alipokuwa kocha wa Sunderland, Di Canio aliendeleza matokeo hayo mazuri kwa kuifunga Everton ikiwa ni mara yao ya kwanza katika mechi 20.
Sasa wamepanda pointi sita kutoka kwenye shimo la kushuka daraja na pia wapo juu ya Newcastle kwa tofauti ya mabao. Di Canio hapa si tu amekubalika, bali anapewa heshima zote za kishujaa.
Lakini, ni jambo gumu kwao kushindwa kushawishika kutokana na ushawishi wa kocha huyo binafsi. Hata wachezaji ambao alifuta mapumziko yao kufurahia matunda ya kazi yao nzuri, wamekuwa wakitii amri na kufuata sera zake.
Viongozi wamekuwa akihangaika juu ya kuwavutia wengi na wakati hizo zikiwa siku za mwnzo kabisa katika fungate lake hapo, lakini Di Canio amewafanya mashabiki wa Sunderland kula kupitia kiganja chake kwa sasa – licha ya kwamba bado hajafanya makubwa kwenye mazoezi ya kikosi hicho.
“Ni muhimu, muhimu sana, hii ni dhamira, kujitolea, kujitoa,” alisema Di Canio baada ya bao la Stephane Sessègnon katika dakika za mwisho za kipindi cha kwanza kuipa Sunderland ushindi wake wa kwanza dhidi ya Everton tangu 2001.
“Imani inaweza kuhamisha milima, katika kila kitu, katika kazi yoyote. Ni jambo muhimu, lakini unapaswa kuwa na imani kama mwanasoka, unahitaji kuwa na jambo hilo kwa wiki yote, si Jumamosi tu.
“Katika vipindi vya mazoezi, Kwa saa moja na nusu au mbili, ni muhimu kuonyesha imani hiyo, kujitolea na dhamira. Dhamira ya kuwa tayari kwa lolote. Kama upo tayari kwa lolote unaweza kutosheka hata kama kuna ugumu. Unapaswa kufanya kazi.”
Di Canio amekuwa akitumia misemo ya kale, lakini umeweza kufanya kazi hadi zama hizi za sasa.
Akipewa nafasi ya kuchukua mikoba ya Martin O’Neill huku kukiwa kumebaki mechi saba, hiyo ilionekana kama kucheza kamari, lakini kwa kipindi kifupi ameweza kudhihirisha ubora wake.
Kulikuwa na nyakati klabu hiyo ilikuwa haina cha kuzungumza, lakini kwa sasa wana mambo mengi yanayovutia na ukitazama staili za ushangiliaji wa kocha zinavutia na kama ingekuwa filamu basi hakika ingefanya vizuri sana kwenye mauzo.
No comments:
Post a Comment