STAA wa filamu za Kibongo, Ahmed Uloto ‘Mzee Chilo’
amewachana wasanii wa filamu wanaovaa nusu uchi huku akieleza kuwa, kufanya hivyo
ni kuihaibisha tasnia ya filamu Bongo.
Akizungumza na jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Mzee
Chilo alisema amekuwa kwenye tasnia hiyo kwa muda mrefu sana na kuwashudia
wasanii kama vile Suzan Lewis ‘Natasha’ na mama Mjata wakiigiza filamu zao
kiheshima lakini siku hizi anashangazwa na uvaaji unaokiuka maadili, si kwenye
filamu tu bali hata kwenye maisha yao ya kila siku.
“Mbona kuna hawa wakongwe
ambao wanaigiza vizuri na kufikisha ujumbe bila kuvaa nusu uchi? Kwa kweli hali
sasa hivi ni mbaya na wasanii hasa wa kike wanatakiwa kujirekebisha wanapokuwa
wanaigiza na hata kwenye maisha yao ya kawaida,” alisema Mzee Chilo.
No comments:
Post a Comment