Hali ya
sherehe ilitaanda katika mbio za marathon za London Jumapili licha ya kuwepo na wasiwasi kufuatia
mashambulizi ya bomu wiki iliyopita katika mbio za marathon za Boston nchini
Marekani.
Siku sita
baada ya mashambulizi hayo karibu na mstari wa kumalizia kwenye mji wa Boston ,
wakimbiaji huko London walituma ujumbe wenye nguvu wa umoja kwa wakazi wa jimbo
wa kaskazinimashariki la Marekani na waathiriwa.
Raia wa
Ethiopia Tsegaye Kebede, alishinda mbio
za wanaume akimaliza kwa kutumia saa mbili
na dakika sita na sekunde nne.
Priscar
jeptoo kutoka Kenya aliibuka mshindi katika mbio za wanawake kwa kumaliza mbio
za kilomita 45 kwa kutumia saa 2 kadika 20 na sekunde 15.
Takriban
wakimbiaji elfu 34 walishiriki mjini London. Waandaaji waliahidi kuchangia dola
tatu kwa kila mkimbiaji aliyemaliza, katika
fuko la Boston lililoanzishwa
kwaajili ya waathiriwa wa mabomu huko Boston.
No comments:
Post a Comment