Mwaite Juma wa Chalinze kushoto akimwangalia bondia Mussa Ali baada ya kupiga konde zito na kwenda chini
ZAIDI ya
mashabiki 300 wamejitokeza kuangalia mpambano wa Masumbwi kwa ajili ya
kuhamasisha mchezo wa ngumi Chalinze
Mkoa wa Pwani pamoja na vitongoji vyake mashindano hayo ya masumbwi
yaliyoandaliwa maalumu kuhamasisha mchezo huo katika vitongoji maarufu.
Uliwakutanisha
mabondia wa Dar es salaam na Chalinze na mabondia wanaotamba katika kitongoji
hicho mpambano huo wa masumbwi ulioanza saa tatu ya usiku na kumalizika saa nne
na nusu uliwakutanisha bondia Amos Thomas aliye toka sare na Andrew Joseph huku
mpambano mwingine ukiwakutanisha Zumbe Kukwe wa Dar es salaam aliye mgalagaza
bila huruma Said Minyusi wa Chalinze
Mpambano
mwingine ni Alex Kado wa Chalinze alishindwa kuhimili mikiki mikiki ya Nassoro
Khatibu na kupigwa kwa pointi
Pambano
lililokuwa likisubiriwa na watu wengi zaidi ni mpambano uliowakutanisha Mwaite
Juma wa Chalinze na Mussa Ali ambapo Mwaite aliweza kumsambaratisha Ali kwa TKO
ya raundi ya kwanza na kupeleka shwangwe kwa wapenzi waliojitokeza katika
mpambano huo
Baada ya
kumalizika kwa mpambano huo Diwani wa Kata ya Bwilingi Chalinze Ahmed Kalama
Nassar ambaye alikuwa mgeni rasmi wa mpambano huo alisema yupo tayari
kuwanunulia vifaa vya mchezo huo ili kuendeleza masumbwi katika kata hiyo
Ambapo ameahidi
kuongeza ushirikiano wa wataalamu wa masumbwi kwa kushirikiana na viongozi ili
Chalinze kiwe kitovu cha masumbwi nchini
|
No comments:
Post a Comment