Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, April 11, 2013

FC BASEL YAITUPA NJE TOTTENHAM HOT SPURS KWA PENALTI 4-1 BAADA YA KUTOKA SARE YA 2-2 KWENYE EUROPA LEAGUE

Tottenham Wakicheza Ugenini Uswisi ndiyo walianza kufunga bao dakika ya 23 kupitia kwa mchezaji wao Clint Dempsey aliyeotea na kuwanyemelea Basel bila kuwa na Habari na kumchenga kipa na kufunga bao hilo.
Nayo Basel wakasawazisha bao hilo kwa kuwashtukizia Spurs ndani ya dakika nne kupitia kwa mchezaji wao Mohamed Salah. 
Tottenham walitinga bila ya Wachezaji muhimu ambao ni majeruhi na ambao ni Gareth Bale, Aaron Lennon na William Gallas kwenye mechi hii wamefungwa tena bao jingine kipindi cha pili dakika ya 49 na Aleksander Dragovic. Dakika ya 82 Clint Dempsey akaipachikia bao jingine Spurs la kusawazisha na kuwa 2-2. Dakika 90 zikamalizika na kuongezewa muda wa dakika 30. Hatimaye dakika 30 kuisha bila ya kufungana, mikwaju ya penati kufata. Spurs wakiondolewa nje ya mashindano haya kwa mikwaju ya penati kwa jumla ya 4-1.

 Clint Dempsey akikimbia kwa kushangilia baada ya kuwafunga bao Basel dakika ya 23 ya mchezo

Wachezaji wa Spurs wakimpongeza Clint kwa kuwapatia bao

Massadio Haidara akijaribu kumpita  Andre Almeida kwa kumzunguka ili apate mpira
Ilikuwa kama bahati mbaya kwa Spurs dakika chache tu kupita mchezaji wa Basel Mohamed Salah akawachoma bao la kusawazisha na kufanya 1-1
Wachezaji wa  Basel wakipongezana mara baada ya Salah kuwasawazishia bao dakika ya 27

Lewis Holtby na Emmanuel Adebayor wakionekana kushoka baada ya kusawazisha Basel bao na kuwa 1-1
Emmanuel Adebayor akimchenga mchezaji wa Basel  Valentin Stocker
Still in with a shout: Clint Dempsey celebrates after levelling the match at 2-2
Clint Dempsey akishangilia baada ya kusawazisha bao na kufanya 2-2

VIKOSI:
FC Basel 2 Tottenham Hotspur 2 (Agg: 4-4)
Basel: Sommer, Philipp Degen, Schar, Dragovic, Park, El-Nenny, Fabian Frei, Die (Diaz 58), Salah (Alexander Frei 110), Stocker (Steinhofer 70), Streller
Substitutes not used: Vailati, David Degen, Cabral, Sauro
Scorers: Salah, Dragovic 
Tottenham Hotspur: Friedel, Walker, Dawson, Vertonghen, Naughton (Assou-Ekotto 77), Dembele (Carroll 58), Parker (Huddlestone 77), Holtby, Dempsey, Sigurdsson, Adebayor
Substitutes not used: Lloris, Livermore, Caulker, Coulthirst
Scorer: Dempsey 2
Booked: Naughton, Dembele
Sent off: Vertonghen 
Referee: Olegario Benquerenca (Portugal)

No comments:

Post a Comment