


Lakini Sunderland baada ya kuwatandika watani zao wa jadi Newcastle wikiendi iliyopita kwa mabao 3-0, Jana walikuwa nyumbani kwenye viunga vya Stadium of Light kuwakaribisha Everton.

Kwa mara nyingine, Kocha muitaliano Paulo Di Canio aliendelea kuwapa furaha mashabiki wa Sunderland baada ya kuiongoza timu hiyo kupata ushindi wa pili mfululizo dhidi ya Everton.
Stephane Sessegnon ndiye alikuwa shujaa wa jana,ambaye alifunga bao la pekee kwa Sunderland kwa shuti kali lililoshindwa kudakwa na Tim Howard mlinda mlango wa Everton, Dakika chache kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika.

Hii imekuwa mara ya kwanza kwa Sundeland kuifunga Everton tangu mwaka 2001 kwenye ligi kuu soka nchini England ambapo mara ya mwisho ilikuwa miaka 12 iliyopita katika msimu wa ligi ambayo Di Canio alikuwa mchezaji wa West Ham United.

Matokeo hayo yanaifanya Sunderland kupanda hadi nafasi ya 14 kwenye msimamo wa ligi wakiwa na pointi 37, lakini kocha Di Canio anasema bado timu hiyo ipo kwenye wakati mgumu na anahitaji kuona anapata ushindi kwenye michezo yote iliyosalia.


Marouane Fellaini kwenye patashika jana jioni.

Seamus Coleman akichuana na James McCleanj uu kwa juu

Colback na Pienaar wakichuana kuugombea mpira

Di Canioakiendeleza majanga kwa Everton

Mashabiki wa Sunderland wakinyoosha jezi ya Di Canio, kumbuka kocha huyu mpya wa Sunderland alikuwa mchezaji miaka ya 2001 wa klabu ya West Ham United enzi hizo.

Mashabiki wa Sunderland wakionesha love za ukweli kwa kocha wao mpya Paolo di Canio baada ya kuwapa ushindi wa mara ya pili na wa utamu kweli kweli. Ambapo amewawezesha kupanda juu na kuwa nafasi ya 14 wakiwa na alama 37 na mchezo wa 34 na kubakiza mitanange 4. bukobasports.com inakupongeza Di Canio!!

Yo
No comments:
Post a Comment