Vita kusaka tiketi
ya kusafiri kwenda jijini London kwenye mchezo wa fainali wa klabu bingwa
barani Ulaya inaanza usiku huu kati ya Mabingwa wa soka nchini Ujerumani dhidi
ya inayotajwa kuwa timu bora kwa vilabu vya soka duniani kwa wakati huu FC
Barcelona.
Messi
hajacheza mchezo wowote wa Barcelona toka alipoingia kama mchezaji wa akiba na
kuisaidia timu yake kufuzu nusu fainal katika mchezo robo fainali dhidi ya
Paris St-Germain ya Ufaransa. Lakini kuna kila dalili Muanjetina huyo mwenye
umri wa miaka 25 ambaye ndiye mchezaji bora wa dunia kwa sasa,akajumuishwa
kwenye kikosi cha Barcelona kwenye mchezo wa usiku wa leo.
Mwezi
uliopita Messi aliweka rekodi kwenye ligi ya Hispania kwa kuwa mchezaji
aliyezifunga timu zote zinazoshiriki ligi kuu nchini humo maarufu kama La Liga
kwa misimu miwili mfululizo.
Barcelona
inapambana kutaka kutwaa taji la tatu la klabu bingwa barani Ulaya ndani ya
miaka mitano,Huku Bayern Munich ambao msimu ujao watakuwa chini ya aliyekuwa
kocha wa Barcelona, Pep Guardiola, wao wanapambana kutafuta nafasi ya kucheza
fainali yao ya tatu ndani ya miaka minne
No comments:
Post a Comment