Diwani wa Kata ya Bwilingu Chalinze
Bagamoyo,Ahmed Karama Nassar, amekubali kushirikiana na wadau wa mchezo wa
ngumi waweze kupata ukumbi maalumu wa mchezo huo.
Chalinze ambaye alikuwa mgeni rasmi alitoa
kauli hiyo jana kwenye mapambano ya ngumi uliopigwa katika ukumbi wa CCM
Mwijuma, Mwananyamala, jijini Dar es Salaam.
“Nitarajia kuuletea maendeleo mchezo
huu kwa kuwa mmenishawishi kuupenda japo wadhamini wachache ndio wanaojitokeza”,
alisema Karama.
Pia alisema ameandaa mpambano utakaochezwa Chalinze kwa
ajili ya kuhamasisha mchezo huo April 21, mwaka huu na kuwaomba wadau wote wa
ngumi wafike Chalinze, wasaidie kuhamasisha mchezo huu
Kwenye pambano hilo mabondia toka
Dar es Salaam ambao watapambana na mabondia wa Chalinze hivyo kutakuwa na
ushindani mkubwa na ameahidi usafiri wa kuwapeleka Chalinze mabondia na
mashabiki watakaopenda kwenda.
Karama kwa kudhihirisha kuwa
amepania kuendeleza ndondi alitoa pesa taslimu shilingi 1,500,000 kwa ajili ya
malipo ya baadhi ya mabondia waliokuwa hawajilipwa na kuanza kudai kugoma
kupanda ulingoni juzi.
Mdau wa ngumi Ibrahimu Kamwe
amempongeza Karama na kuomba watu na viongozi wengine waige mfano wake na
kuahidi hata Chalinze atakwenda kushuhudia pambano hilo
No comments:
Post a Comment