Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, March 31, 2013

YANGA, SIMBA ZABANWA, AZAM YAIVUTIA KASI YANGA


 Ikiwa mkoani Morogoro jana ikicheza dhidi ya maafande wa Polisi vinara wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara Yanga wamelazimishwa sare ya bila kufungana mchezo uliopigwa katika dimba la Jamhuri mkoani humo.

Sare hiyo imeifanya Yanga kuambulia alama moja tu ambayo imewafanya kufisha jumla ya 49 katika msimamo wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara.

Yanga ilielekea katika mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa bao 1-0 iliyoupata kwa Ruvu shooting ya Pwani.
 Yanga sasa imesaliwa na michezo minne ya ligi hiyo kabla ya kufikia tamati huku mchezo dhidi ya watani wao wakubwa katika soka la Tanzania ukitarajiwa kuchezwa mei 18.

Mchezo ujao Yanga itakuwa ikicheza dhidi ya JKT Oljoro Aprili 10 kabla ya kuifuata Mgambo JKT mkoani Tanga siku tatu baadaye.

Itarejea tena Dar es Salaama kukabiliana na Coast Union siku ya May mosi kabla ya kumsubiri mpinzani wake Simba mei 18.

Wenyewe Simba walilazimishwa sare ya mabao 2-2 na Toto Afrika ya Mwanza  katika mchezo uliofanyika katika dimba la CCM Kirumba Simba kuongeza alama moja na sasa wakiwa na 35 

Katika mchezo ujao Simba watakuwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kukabiliana na wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kombe la Shirikisho Azam fc walio katika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi.

Kwenye uwanja wa Sheikh Karume Arusha JKT Oljoro waliifunga JKT Ruvu mabao 2-0.

Azam hii wamevuna alama tatu muhimu mbele ya Ruvu Shooting baada ya kuchomoza na ushindi wa bao 1-0 bao lililofungwa na mshambuliaji hatari Kipre Tchetche  mchezo uliofanyika uwanja wa Mabatini Mlandizi mkoani Pwani.

 Kwa ushindi wa leo wa Azam fc imefikisha jumla ya alama 43 ikiwa ni alama sita nyuma ya vinara Yanga wenye alama 49.

No comments:

Post a Comment