Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, March 24, 2013

SIMBA YABANWA MBAVU NA RHINO RANGERS YATOKA 1-1




WEKUNDU wa Msimbazi, Simba jana wamelazimishwa sare ya kufungana na 1-1 na Rhino Rangers ya Tabora iliyopanda Ligi Kuu katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi, Tabora.

Mchezo huo ulikuwa  maalum kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar mjini Bukoba Jumatano.
Simba SC ambayo katika mchezo wake uliopita wa kirafiki iliifunga Singida United mabao 4-0, katika mchezo wa  jana, bao lake limefungwa na Edward Christopher kwa njia ya penati. dakika ya 25 na bao la Rhino rangers lilifungwa na Abdalah Simba dakika ya 35 kipindi cha kwanza

Katika mchezo uliopita uliofanyika kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida, mabao ya mabingwa hao wa Bara, yalitiwa kimiani na Rama Kipalamoto, Mselemu Salum, Omar Waziri ‘Inzaghi’ na Ramadhani Singano ‘Messi’.

Simba SC ambayo imewapumzisha wachezaji wake wengi wa kikosi cha kwanza na kuamua kutumia chipukizi waliopandishwa kutoka kikosi cha pili,  ilicheza soka ya kuvutia na kupoteza nafasi kadhaa za kufunga mabao zaidi.

Kocha Mfaransa, Patrick Liewig alitoa pendekezo la kutolewa kwa wachezaji ‘mafaza’ katika kikosi chake, kwa kuwa hawamsikilizi.
Miongoni mwa waliotengwa ni wachezaji hodari na vipenzi vya mashabiki kama Amir Maftah, Juma Nyosso, Haruna Moshi ‘Boban’ na Mwinyi Kazimoto.

Wachezaji hao makinda walicheza mechi ya kwanza ya Ligi Kuu wiki mbili zilizopita dhidi ya Coastal Union ya Tanga na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Sasa timu hiyo inaelekeza nguvu zake katika mechi mbili za kanda ya Ziwa, ikianza na Kagera na baadaye Toto African mjini Mwanza wiki ijayo, huku wapenzi wengi wakiwa na imani na yosso wao hao.

Simba itaondoka kesho asubuhi kuelekea Bukoba tayari kwa mechi na Kagera Jumatano.
Kwa sasa, Simba SC inashika nafasi ya tatu katika Ligi Kuu, ikiwa na pointi 34, tatu nyuma ya Azam FC inayoshika nafasi ya pili wakati Yanga SC wapo jirani kabisa na ubingwa kwa pointi zao 48 ligi ikiwa imebakiza mizunguko sita kutia nanga.

Simba SC inapambana hata kama itapoteza ubingwa, basi iipiku Azam FC katika nafasi ya pili.
Katika mchezo wa jana, kikosi cha Simba kilikuwa; Abuu Hashim, Emily, Hassan Hassan, Hassan Khatib, Jonas Mkude, Ndemla, Abdallah Seseme, Rashid Ismail, Christopher Edward, Ramadhani Singano ‘Messi’ na Haroun Chanongo.

No comments:

Post a Comment