MABONDIA PRINCE NAIDJALA NA SEKOTSWE NUSU WAZIPIGE KAVU KAVU
Immanuel "Prince" Naidjala
Mabondia Immanuel “Prince” Naidjala wa Namibia
and Lesley Sekotswe wa Botswana wamekutana leo katika mkutano wa waandishi wa
habari. Kukutana kwao nusura kulete balaa kubwa baada ya mabondia wenyewe
kuingia midadi na kutaka kuzipiga kavu kavu mbele ya vyombo vya habari.
Mkutano huo ulifanyika katika hotel ya Windhoek Country Club Resort ambayo ni
moja ya Casino kubwa katika nchi ya Namibia. Vyombo mbalimbali vya habari
kutoka nchi za Afrika na Ulaya zilishiriki katika mkutano huo ambao wawili hao
walitambiana kupeana mkongoto wa uhakika watakapokutana Machi 20 mwaka huu,
Mabondia hao wanakutana tena kesho tarehe 19 katika hoteli hii katika zoezi la
kupima uzito kabla ya mpambano wao siku ya Jumatano ambayo ni siku ya Uhurru wa
nchi ya Namibia. Viongozi wakuu wa serikali ya Namibia watahudhuria mpambano
huo ambao ni mkubwa kuwahi kufanyika katika nchi hii yenye wakazi milioni mbili
na ushee!
Naye Rais wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati
Mtanzania Onesmo Ngowi amewasili jijini Windhoek leo akitokea nchini Ghana
kulisimamia pambano hili la ubingwa wa “IBF International Title”
Rais Ngowi ametokea jijini Accra, Ghana ambapo alishughudia mabondia Richard
Commey na Bilal Mohammed wakitoana jasho ambako Richard Commey aliibuka kuwa
bingwa wa uzito mwepesi katika bara la Afrika.
Promota wa mpambano huo Nestor Tobias wa kampuni maarufu ya Sunshine Boxing
Promotions ana uhakika wa mpambano huu kuvunja rekodi ya kuingiza watu wengi
zaidi ya mapambano yote yaliyowahi kufanyika nchini Namibia.
Pambano hili litawakutanisha pia baadhi ya mabondia kadhaa katika mapambano ya
awali ambako bondia Martin Haikali wa Namibia atakutana na Nelson Banda wa
Zambia katika mpambano wa raundi 8
Mkutano huo ulifanyika katika hotel ya Windhoek Country Club Resort ambayo ni moja ya Casino kubwa katika nchi ya Namibia. Vyombo mbalimbali vya habari kutoka nchi za Afrika na Ulaya zilishiriki katika mkutano huo ambao wawili hao walitambiana kupeana mkongoto wa uhakika watakapokutana Machi 20 mwaka huu,
Mabondia hao wanakutana tena kesho tarehe 19 katika hoteli hii katika zoezi la kupima uzito kabla ya mpambano wao siku ya Jumatano ambayo ni siku ya Uhurru wa nchi ya Namibia. Viongozi wakuu wa serikali ya Namibia watahudhuria mpambano huo ambao ni mkubwa kuwahi kufanyika katika nchi hii yenye wakazi milioni mbili na ushee!
Naye Rais wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati Mtanzania Onesmo Ngowi amewasili jijini Windhoek leo akitokea nchini Ghana kulisimamia pambano hili la ubingwa wa “IBF International Title”
Rais Ngowi ametokea jijini Accra, Ghana ambapo alishughudia mabondia Richard Commey na Bilal Mohammed wakitoana jasho ambako Richard Commey aliibuka kuwa bingwa wa uzito mwepesi katika bara la Afrika.
Promota wa mpambano huo Nestor Tobias wa kampuni maarufu ya Sunshine Boxing Promotions ana uhakika wa mpambano huu kuvunja rekodi ya kuingiza watu wengi zaidi ya mapambano yote yaliyowahi kufanyika nchini Namibia.
Pambano hili litawakutanisha pia baadhi ya mabondia kadhaa katika mapambano ya awali ambako bondia Martin Haikali wa Namibia atakutana na Nelson Banda wa Zambia katika mpambano wa raundi 8
No comments:
Post a Comment