Bondia Francis Cheka amepata pigo la mwaka kwenye pambano la ubingwa wa IBF Inter-continental nchini Ujerumani baada ya mtu mmoja kutoka katika kona yake kurusha taulo uwanjani (ikiwa ni ishara ya kusimamisha pambano) na kusababisha mwamuzi kumaliza mchezo hivyo Mjerumani Uensal Arik kupewa ubingwa.
Katika pambano hilo, Cheka alimkabili vilivyo mpinzani wake Arik hadi raundi ya saba zikiwa zimebakia sekunde 15, ndipo mmoja wa watu wa kona yake aliporusha taulo kuashiria kuomba mwamuzi asimamishe pambano ili kumnusuru bondia huyo.
Kitendo hicho kilimkasirisha Cheka na kuanza kugombana na watu wa kona yake kwa kuamua kumaliza pambano kwa namna hiyo.
Wakati mwamuzi anasimamisha pambano Cheka alikuwa akiongoza kwa pointi 57-56, 57-56 na 58-56 alizokusanya kwenye raundi sita za kwanza.
Cheka alitawala vizuri raundi mbili za kwanza na kufanikiwa kumwangusha chini Arik kwenye raundi ya tano, lakini Mjerumani huyo aliokolewa na kengele wakati mwamuzi akimhesabia.
Arik aliamka mwanzoni mwa raundi ya sita, lakini mwishoni Cheka alibadilika na kutawala.
Raundi ya saba Arik aliingia kama kichaa, lakini Cheka alikuwa makini kumkabili ghafla taulo likarushwa ulingoni zikiwa zimebaki sekunde 15 na kuharibu pambano hilo.
Raundi ya saba Arik aliingia kama kichaa, lakini Cheka alikuwa makini kumkabili ghafla taulo likarushwa ulingoni zikiwa zimebaki sekunde 15 na kuharibu pambano hilo.
No comments:
Post a Comment