Mwenyekiti wa Chama cha Soka Dar es Salaam Almas Kasongo (anayezungumza) aliyeko pembeni ni Mwenyekiti wa IDFA, Daudi Kanuti |
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
12thMARCH 2013
Kamati ya Utendaji ya Chama Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam kwa mamlaka iliyonayo imeteua kamati mbali mbali zitakazoshirikiana na Kamati ya Utendaji katika kukabiliana na changamoto mbali mbali za mpira wa miguu katika Mkoa wake ili kuweza kufikia malengo yake waliyojiwekea. Wafuatao ni watu na kamati mbali mbali walioteuliwa/zilizoteuliwa na Kamati ya Utendaji ya Chama Cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam:
Bw. Joseph Kanakamfumo Mkurugenzi wa Ufundi
Bw. Saidi Pambalelo Afisa Tawala
Bw. Mohamedi Muharizo Afisa Habari
Bw. Hashim Abdallah Afisa Usalama
KAMATI YA FEDHA NA MIPANGO
1. Bw. Meba Ramadhani Mwenyekiti
2. Bw. Iddi Msonga Makamu Mwenyekiti
3. Bw. Ali Hassani
4. Bw. Ramadhani Kilemile
5. Bw. Isack Mazwile
KAMATI YA UFUNDI NA MASHINDANO
1. Bw. Kenny Mwaisabula Mwenyekiti
2. Bw. Shabani Mohamedi Makamu Mwenyekiti
3. Bw. Hugo Seseme
4. Bw. Daudi Kanuti
5. Bw. Kassim Mustapha
6. Bw. Abeid Mziba
7. Bw. Bakari Mtumwa
KAMATI YA MAENDELEO YA SOKA LA VIJANA NA WANAWAKE
1. Bw. Benny Kisaka Mwenyekiti
2. Bw. Muhsin Balhabou Makamu Mwenyekiti
3. Dr. Sesy Makafu
4. Bw. Emmanuel Kazimoto
5. Dr. Maneno Tamba
6. Bw. Edwin Mloka
7. Bw. Sande Mwanahewa
8. Bw. Richard Shayo
KAMATI YA WAAMUZI
1. Bw. Jovin Ndimbo Mwenyekiti
2. Bw. Sijali Mzeru Makamu Mwenyekiti
3. Bw. Saidi Mbwana
4. Bw. Benny Mtula
5. Bw. Abdallah Mitole
KAMATI YA NIDHAMU NA USULUHISHI
1. Mheshimiwa Roman Masumbuko Mwenyekiti
2. Bw. Fahadi Faraji Kayuga Makamu Mwenyekiti
3. Bw. Mohamedi Mpili
4. Bw. Peter Nkwera
5. Bw. Jimmy Mhango
KAMATI YA RUFAA
1. Mheshimiwa Salehe Njaa Mwenyekiti
2. Bw. Saidi Engo Makamu Mwenyekiti
3. Bw. Abasi Kuka
4. Bw. Yusuph Macho
5. Bw. Boi Risasi
Pia Kamati ya Utendaji ya Chama Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam inapenda kuwafahamisha wanachama wake, wadau na mashabiki wa mpira wa miguu Tanzania dhamira yao ya kuendeleza mpira wa miguu katika Mkoa wa Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla.
Kwa kuanzia Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam kipo kwenye mchakato wa kukamilisha DRFA Strategic Plan 2013 - 2016 (Mpango Mkakati Kazi) kwa kipindi cha miaka minne pamoja na kuboresha Financial Regulations zake ili kiweze kuwa na dira ya kuwahudumia wadau wake kwa ufanisi na uwazi zaidi. Lakini pia Kamati ya Utendaji imeona haja ya Chama Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam kuwa na Websiteyake kwa ajili ya kuwapa habari wadau wake na Watanzania kwa ujumla.
Mwisho Kamati ya Utendaji ya Chama Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam kinaomba ushirikiano na wadau wote wa mpira hususani Serikali, TFF, Vyama vya Mikoa, Walimu, Waamuzi, Madaktari, Vilabu, Makampuni na Waandishi wa habari na Vyombo vya habari katika kuendeleza mpira wa miguu katika mkoa wa Dar es Salaam na hatimaye mikoa yote ya Tanzania. “Kwani Pamoja Tunaweza”
Ahsanteni,
Almasi Kasongo
Mwenyekiti wa Chama Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)
No comments:
Post a Comment