Timu zote zimecheza kwa kukamiana
Russia wakianza kwa mashambulizi makali na kukosa magoli mengi kipindi cha
kwanza cha dakika ya kwanza mpaka ya 15 na kupata kona nyingi, huku Brazil nao
wakiongoza robo ya kipindi cha mwisho cha kwanza
cha dakika 45 na hatimaye kipindi cha kwanza kuisha timu zote zikiwa zinatoshana nguvu bila ya kufungana.Huku wachezaji wawili
Kerzhakov na Shirokov wakionesha kuwa hatari sana kuongoza mashambulizi kwenye
timu ya Brazil.Pia kipindi hiki cha kwanza
kuanzia dakika ya 36 Brazil waliongoza kwa mashabulizi kwa Russia ambao
walionekana kuchoka na mashambulizi hayo yakiongozwa na kaka pamoja na Oscar.
kipindi cha pili Brazil walianza tofauti na
kipindi cha kwanza, Wameanza kwa kuiandama Russia
mpira ukipaki mbele kwenye eneo la goli la Russia
na katikati na wakikosa pia magoli ya wazi
Brazil.Mashambulizi yakiongozwa na Kaka, Neymar pamoja na
Oscar. Kipindi cha pili dakika ya 66 Brazil
wakafanya mabadiliko wakamtoa Oscar na nafasi yake ikachukuliwa
na Hulk. Dakika
ya 73 wachezaji wa Russia wakabomoa ngome ya Brazil akiwemo Thiago Silva, Dani
Alves, Marcelo na na hatimaye mchezaji Viktor Faitzulin kutofanya makosa na
kuutokomezea nyavuni ambapo ulimkuta David Luiz akiwa hoi na mpira kumpita
pembeni hadi nyavuni. Dakika ya 78 Brazil wakafanya mabadiliko tena wakamuingiza
mchezaji straika wa Atletico Madrid Diego
Costa wakimtoa Kaka ili aweze kuziba pengo hilo. Dakika za lala salama 90' mchezaji Hulk kushirikiana na mchezaji Marcelo
wakaingia nao kwenye ngome ya Russia
na hatimaye mchezaji Fred akausogezea mpira nyavuni na
kuwasawazishia bao na
kufanya 1-1. Wachezaji wa timu ya taifa ya Brazil, wakishangilia
bao la timu yao ilipoumana na Russia jana usiku.
Victor Fayzulin wa Russia (20) akifunga bao kunako
dakika ya 73 ya pambano la kirafiki dhidi ya Brazil kwenye dimba la Stamford
Bridge jijini London jana usiku.
Victor Fayzulin wa Russia (20) akifunga bao kunako
dakika ya 73 ya pambano la kirafiki dhidi ya Brazil kwenye dimba la Stamford
Bridge jijini London jana usiku.
Wachezaji wa timu ya taifa ya Brazil, wakishangilia
bao la kusawazisha lililofungwa na Fred (katikati).
Mshambuliaji wa Brazil Fred akifunga bao la timu yake
katika mechi hiyo ya kukata na shoka.
Fred, akishangilia bao lake huku akimfuata David Luiz
kupongezana
VIKOSI:
BRAZIL:
12. Júlio César, 2. Dani
Alves,3.Thiago Silva, 4.David Luiz, 6. Marcelo, 5. Fernando, 7. Oscar, 8.
Hernanes, 10. Kaká, 9. Fred, 11. NeymarRUSSIA:
12. Vladimir Gabulov, 2. Aleksandr Aniukov, 4.
Sergei Ignashevich, 14. Vasili Berezutsky, 22 .Andrei Yeschenko, 8 Denis
Glushakov, 15. Roman Shirokov, 18 .Vladimir Bystrov, 20.Viktor Faitzulin,
9. Alexander Kokorin, 11. Alexander
KerzhakovReferee: Howard. Webb
No comments:
Post a Comment