Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, February 14, 2013

WAMBURA AFUNGUKA, AIPA TFF SIKU TATU KUTENGUA MAAMUZI VINGEVYO ANAENDA MAHAKAMANI



KATIBU Mkuu wa zamani wa kilichokuwa Chama Cha Soka nchini (FAT) (TFF), Michael Wambura, anatarajia kutoa tamko lake leo saa sita kamili za mchana, katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo juu ya kuenguliwa kwake kugombea nafasi ya Makamu wa Rais wa Shirikisho hilo, katika Uchaguzi uliopangwa kufanyika Februari 24.
Wambura ameendelea kung’ang’aniwa na wadau wa soka, kwa kumtoa kila anapojaribu kuwania nafasi yoyote katika medani ya mpira wa miguu hapa nchini, ikiwapo TFF.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Wambura alisema kwamba anatafakari pamoja na kupokea barua kutoka TFF juu ya kumuengua kwake kuwania nafasi ya Makamu wa Rais.
Alisema anaitumia nafasi hiyo kukaa na kupitia vifungu mbalimbali vilivyokuwa kwenye Kanuni za TFF, kabla ya kuzungumzia mustakabali wa soka la hapa nchini.
“Sijataka kukurupuka kutoa uamuzi baada ya kusikia kwenye vyombo vya habari kuwa rufaa yangu haijakuwa nzuri baada ya matokeo yale yale ya Kamati ya Uchaguzi kujirudia.
“Naamini nipo tayari leo mchana kuzungumzia yote kwa nia ya kutoa picha kamili ya matokeo ya kuelekea Uchaguzi Mkuu wa TFF utakaofanyika Februari 24,” alisema.
Katika Uchaguzi huo, nafasi pekee ya Urais imebaki kwa mgombea wake, Athumani Nyamlani, baada ya mpinzani wake, Jamal Malinzi naye kutupwa na Kamati ya Rufaa kwa madai hana uzoefu.
 

No comments:

Post a Comment